• HABARI MPYA

    Monday, October 02, 2017

    SERIKALI YAAHIDI KUIPELEKA CUBA TIMU YA TAIFA YA NGUMI KUJIANDAA NA MADOLA 2018

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SERIKALI imeahidi kuipeleka Cuba taifa ya ngumi za Ridhaa Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola mwaka 2018.
    Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Yusuph Singo wakati wa kufunga michezo ya kujipima nguvu ya timu ya taifa kujiandaa na Michezo ya Jumuiya ya Madola mwakani.
    Singo alisema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mpango wa timu ya Taifa ya ngumi kwenda nchini Cuba kwa ajili ya mazoezi ya kushiriki mashindano ya Jumuya ya Madola 2018.
    Singo alisema Serikali imeona na inatambua jitihada zinazofanywa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) katika kuendeleza mchezo huo, hususan katika kuandaa timu ya Taifa mapema kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola 2018.
    Alisema serikali itakuwa karibu na BFT kuhakikisha mazoezi hayo yanaendelea vizuri na kusaidiana kuondoa changamoto zilizopo.
    BFT iliandaa mapambano maalum ya kujipima nguvu kwa mabondia wa timu ya taifa dhidi ya mabondia wa Ngome, timu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lengo likiwa kuwapa mazoezi wachezaji wa timu ya taifa, ikiwa sehemu ya maandalizi ya kushiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Gold Coast, Australia Aprili 2018. 
    Katika mapambano hayo, Herman Shekivuli wa Taifa alimshinda Issa Kpaya wa Ngome uzito wa Fly, Geoge Costantino wa Taifa alimshinda John Christian wa Ngome uzito wa Bantam, Ezra Paul wa Taifa alimshinda Emmanuel Marwa wa Ngome uzito wa Feather na Ismail Galiatana wa Taifa alimshinda Fabian Gaudence wa Ngome uzito wa Light.
    Wengine ni Mohamed Juma wa Taifa aliyemshinda Isiaka Lusajo wa Taifa uzito wa Light Welter, Kassim Butike wa Taifa alimshinda Julius Nickson wa Ngome uzito wa Welter, Selemani Kidunda wa Taifa alimshinda Daudi Kuzenza wa Ngome uzito wa Light Middle na Yusuph Changarawe wa Taifa alimshinda Twalibu Kinyogori wa Ngome uzito wa Middle,
    Haruna Swanga wa Taifa alimshinda Alex Sitta wa Taifa, Alex Michael wa Ngome alimshinda Mwalimu Ngayana wa Taifa, Kelvin Kapinga wa Ngome alimshinda Said Ramadhani wa Taifa na Batele Abed wa Ngome alimshinda Mwinyi Ally.
    Kwa upande wa wanawake, Siwatu Kimbe alimshinda Lusiana Gadani wote wa Taifa, Safina Fussi alimshinda Asha Juma wa Taifa, Najma Isike alimshinda Monica Malango wote wa Taifa, Mariam Macho wa Taifa alimshinda Naomi Shoo wa Taifa, Grace Mwakamale wa Taifa alimshinda Leonia Kalimunju wa Taifa.
    BFT imeahidi kuwa mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila wa kila  mwezi kwa kushindana na timu za ndani na nje ya Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAAHIDI KUIPELEKA CUBA TIMU YA TAIFA YA NGUMI KUJIANDAA NA MADOLA 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top