• HABARI MPYA

    Wednesday, October 11, 2017

    ROBBEN ASTAAFU BAADA YA UHOLANZI KUKOSA KOMBE LA DUNIA

    MKONGWE wa Uholanzi, Arjen Robben ametangaza kustaafu soka ya kimataifa usiku wa jana baada ya kuifungia mabao mawili timu yake dhidi ya Sweden katika mchezo wa Kundi A kufuzu Kombe la Dunia.
    Robben alifunga mabao yote jana Uholanzi ikishinda, lakini ikashindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwakani, baada ya kuzidiwa wastani wa mabao na Sweden kufuatia kulingana kwa pointi 19.
    Winga huyo machachari alikaribia kudondosha machozi jana kabla na baada ya mechi Uwanja wa Amsterdam Arena.
    "Ni wakati mzuri kukabidhi mwenge kwa kizazi kijacho,"alisema.
    Mkongwe Arjen Robben ametangaza kustaafu soka ya kimataifa jana usiku PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Alisema kwamba Uholanzi imeshindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002. "Tulijua kabla ya mchezo huu, itakuwa vigumu kwetu kwenda Kombe la Dunia,".
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, katika kipindi chake cha miaka 14 ya kuichezea timu yake ya taifa, amekuwa mwenye mafanikio, akifunga jumla ya mabao 37 na kutoa pasi za mabao 29 katika mechi 96. 
    Alikuwa tegemeo la Uholanzi ikishika nafasi ya pili katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla ya kumaliza nafasi ya tatu nchini Brazil miaka mitatu iliyopita. 
    Atakumbukwa pia kukosa bao la wazi mno dhidi ya Hispania kwenye fainali Afrika Kusini.
    Kipa Iker Casillas alifanya kazi nzuri mno kuokoa mchomo wa Robben kabla ya Hispania ikienda kushinda 1-0 katika dakika za nyongeza. 
    "Ilikuwa safari ndefu, miaka 14," alisema. "Kumbukumbu yangu ya kwanza pia ilikuwa dhidi ya Sweden mwaka 2004 wakati nilipokuwa mdogo mno. Nilipiga penalti ya ushindi tena mwaka 2004, mashindano yangu ya kwanza,".
    "Nimecheza michuano sita, Euro tatu na Kombe la Dunia tatu na matokeo mazuri yalikuwa mwaka 2010 na 2014.
    "Tulikuwa nchi ndogo na mara moja tulikuwa wa pili na mara moja wa tatu. Tunaweza kujivunia mno hili,"alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROBBEN ASTAAFU BAADA YA UHOLANZI KUKOSA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top