• HABARI MPYA

  Monday, October 23, 2017

  MAPEMA TU, SIMBA TAYARI WAPO ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Simba kimeondoka asubuhi ya leo mjini Dar es Salaam kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Yanga Jumamosi.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba kikosi kimeondoka asubuhi ya leo kwenda visiwani humo.
  “Timu imeondoka leo asubuhi kwenda Zanzibar, tutakuwa huko kwa wiki moja kabla ya kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya mechi,”amesema Manara.    
  Simba imekwenda Zanzibar ikitoka kupata ushindi mnono katika Ligi Kuu, baada ya kuichapa 4-0 Njombe Mji Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kufikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi saba.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hance Mabena, aliyesadiwa na Mohammed Mkono, wote Tanga na Abdallah Rashid wa Pwani, hadi mapumziko, mabao ya Simba yalifungwa na kiungo Muzamil Yassin mawili, Mganda Emmanuel Okwi na Mrundi, Laudit Mavugo ambaye kila mmoja alifunga bao moja.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAPEMA TU, SIMBA TAYARI WAPO ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top