• HABARI MPYA

    Wednesday, October 04, 2017

    MAN UNITED KUUPANUA OLD TRAFFORD UWE WA PILI KWA UKUBWA ULAYA

    Manchester United inataka kuupanua Uwanja wake wa Old Trafford uingize mashabiki 88,000 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    VIWANJA 10 VIKUBWA ZAIDI BARANI ULAYA 

    1. Nou Camp (Barcelona) - mashabiki 99.354
    2. Wembley (London) - mashabiki 90,000
    3. Westfalenstadion (Dortmund) - mashabiki 81,359
    4. Stade de France (Paris) - mashabiki 81,338
    5. San Siro (Milan) - mashabiki 80,018
    6. Bernabeu (Madrid) - mashabiki 81,044
    7. Luzhniki Stadium (Moscow) - mashabiki 81,000
    8. Ataturk Stadium (Istanbul) - mashabiki 76,092
    9. Old Trafford (Manchester) - mashabiki 75,643
    10. Allianz Arena (Munich) - mashabiki  75,000 
    VIONGOZI wa Manchester United wanatazama namna ya kuupanua Uwanja wa Old Trafford uingize mashabiki 88,000.
    Mpango ni kuongezazaidi ya viti 12,000 kutoka vya sasa 75,643 kwa kuongeza ukubwa wa jukwaa la Sir Bobby Charlton, ambalo zamani lilikuwa linajulikana kama Jukwaa la Kusini.
    Tayari Old Trafford ndio Uwanja mkubwa zaidi wa klabu Uingereza, ambao ukipanuliwa utaukaribia wa Wembley unaoingiza watu 90,000.
    Itafanya pia Old Trafford ivizidi ukubwa viwanja vya San Siro, Bernabeu, Stade de France na Westfalenstadion barani Ulaya.
    United imeutilia mkazo mpango huo na ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
    United wakifanikiwa kuupanua Uwanja wao, utakuwa unazidiwa ukubwa na Uwanja wa Nou Camp tu wa klabu ya Barcelona kwa Ulaya, ambao unaingiza mashabiki 99,354.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED KUUPANUA OLD TRAFFORD UWE WA PILI KWA UKUBWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top