• HABARI MPYA

  Tuesday, October 03, 2017

  LUKAKU AZUA HOFU MAN UNITED NA UBELGIJI BAADA YA KUUMIA

  MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku amepelekwa kufanyiwa vipimo na madaktari wa timu ya taifa ya Ubelgiji jana baada ya kuripoti mazoezini kwa majukumu ya kimataifa.
  Mshambuliaji huyo wa Manchester United, ambaye amefunga mabao 15 katika mechi 12 kwa klabu yake hadi sasa msimu huu, inafahamika aliumia katika mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya England Mashetani Wekundu wakishinda 4-0 dhidi ya Crystal Palace na jana hakufanya mazoezi na kikosi cha Ubelgiji.
  Taarifa ya Chama cha Soka Ubelgiji imesema: "Romelu Lukaku amekwenda kufanyiwa kipimo cha MRI, lakini hajapasuka au kupata tatizo lolote kubwa. Katika siku zijazo atafuata programu maalum binafsi ya mazoezi. Hata hivyo bado ni mapema sana kusema hatakuwa fiti kwa mechi na Bosnia na/au Cyprus,".
  Romelu Lukaku aliumia katika mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Crystal Palace Man United ikishinda 4-0 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Akizungumza kabla ya mechi na Palace, Jose Mourinho hakutaka kumtia presha kocha wa Ubelgiji, Roberto Martinez kumpumzisha Lukaku dhidi ya Bosnia na Cyprus baada ya kuwa tayari amefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwakani.
  "Ubelgiji ni majukumu ya Roberto,"amesema Mourinho. "Ni uamuzi wake kumchezesha au hapana. Kiprofesheno siwezi kumzungumzia, kumuambia fanya hivi au fanya vile," amesema Mourinho.
  Wakati huo huo, Lukaku amekanusha kufanya pati na kupiga kelele Beverley Hills Julai mwaka huu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hakutokea mahakamani jana mjini Los Angeles, Marekani lakini wakili wake, Robert Humphreys alifika kumuwakilisha.
  Lukaku alikamatwa Julai 2, siku nane kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 75 kutoka Everton kwenda Old Trafford. 
  Ametakiwa kufika mahakamani Uwanja wa Ndege wa Los Angeles Courthouse Novemba 21.
  Mechi ijayo ya United katika Ligi Kuu ya England itakuwa dhidi ya Liverpool Oktoba 14 baada ya mapumzikoa ya kupisha mechi za kimataifa. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AZUA HOFU MAN UNITED NA UBELGIJI BAADA YA KUUMIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top