• HABARI MPYA

    Sunday, October 22, 2017

    KIKAO CHA KWANZA CHA BODI MPYA YA LIGI ALHAMISI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI mpya ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itafanya kikao chake cha kwanza Alhamisi, Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
    Moja ya ajenda katika kikao hicho ni kuteua Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, na kamati nyingine mbalimbali.
    TPLB ilifanya uchaguzi Jumapili, Oktoba 15 mwaka huu na kupata uongozi mpya chini ya Mwenyekiti wake Clement Sanga.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Clement Sanga ataendesha kikao cha kwanza Alhamisi

    Viongozi wengine waliochanguliwa ni Shani Mlingo (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe Hamisi Madaki, Ramadhani Mahano, Almasi Kasongo na Egdar Chibura.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIKAO CHA KWANZA CHA BODI MPYA YA LIGI ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top