• HABARI MPYA

  Monday, October 23, 2017

  KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA YANGA 10,000 MECHI SHAMBA LA BIBI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIINGILIO cha chini katika mchezo wa mahasimu wa jadi, Simba na Yanga utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Oktoba 28, kitakuwa ni Sh 10,000.
  Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam kwamba kiingilio hicho kitahusu majukwaa ya mzunguko ya Uwanja huo, wakati jukwaa kuu watu watalipa Sh. 20,000. 
  Kidau amesema kwamba utaratibu maalum umewekwa kuhakikisha idadi inayotakiwa ya watu 22,000 ndiyo wanaoingia uwanjani kwa kuhakikisha haziuzwi tiketi zaidi.
  Aidha, kiungo huyo wa zamani wa Simba SC, amesema kwamba imelazimika mchezo huo kufanyika Uwanja wa Uhuru kwa sababu Uwanja mkubwa wa Taifa upo kwenye ukarabati.
  Kidau pia amesema kwamba Alhamisi wiki hii Kamati mpya ya Uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) ya TFF itafanya kikao chake cha kwanza mjini Dar es Salaam, kubwa likiwa ni maandalizi ya mchezo huo.
  Lakini pia, Kidau amesema kwamba ajenda nyingine katika kikao hicho ni kuteua Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, na Kamati nyingine mbalimbali.
  Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau amesema kiingilio cha chini Simba na Yanga ni Sh. 10,000 

  Hiyo ni baada ya uchaguzi wa TPLB uliofanyika Jumapili ya Oktoba 15 mwaka huu na kupata uongozi mpya chini ya Mwenyekiti wake Clement Sanga.
  Viongozi wengine waliochanguliwa ni Shani Mlingo (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe Hamisi Madaki, Ramadhani Mahano, Almasi Kasongo na Edgar Chibura.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA YANGA 10,000 MECHI SHAMBA LA BIBI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top