• HABARI MPYA

    Saturday, October 07, 2017

    IVORY COAST MGUU NJE, MGUU NDANI KOMBE LA DUNIA MWAKANI

    TIMU ya Mali imeondolewa kabisa kwenye mbio za kufuzu Kombe la Dunia baada ya sare ya 0-0 na Ivory Coast kwenye mchezo wa Kundi C usiku wa jana Uwanja wa Machi 26 mjini Bamako.
    Matokeo hayo yanaifanya Ivory Coast iendelee kuongoza msimamo wa kundi hilo, huku ikiendela kushika mkia.
    Ivory imemaliza na pointi nane katika mechi ya kwanza, lakini italazimika kusubiri matokeo ya mchezo kati ya Morocco yenye pointi na Gabon tano kujua mustakabli wake wa kwenda Urusi mwakani.   
    Morocco wataikaribisha Gabon Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca kuanzia Saa 4:00 usiku pia.
    Mechi nyingine za leo, Uganda wataikaribisha Ghana Uwanja wa Taifa wa Nelson Mandela, eneo la Namboole mjini Kampala na Misri wakiwa wenyeji wa Kongo Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
    Afrika Mashariki ina matumaini ya kupeleka timu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kihistoria iwapo Uganda itaifunga Ghana na Kongo ikaifunga Misri. Mafarao wanaongoza Kundi E kwa sasa kwa pointi zao tisa, wakifuatiwa na The Cranes pointi saba, wakati Kongo yenye pointi moja inashika mkia. 
    Afrika Kusini inayoshika mkia Kundi D kwa pointi yake moja, itakuwa mwenyeji wa Burkina Faso yenye pointi sita kileleni Uwanja wa FNB mjini Johannesburg. Mechi nyingine ya kundi hilo ni kati ya Senegal yenye pointi tano na Cape Verde pointi sita.
    Nigeria yenye pointi 10, itahitaji sare tu mbele ya Zambia yenye pointi saba Uwanja wa Godswill Akpabio kujihakikishia nafasi ya kwenda Urusi mwakani katika mchezo wa Kundi B. Mechi nyingine ya kundi hilo ni ya kukamilisha ratiba kati ya Cameroon yenye pointi tatu na Algeria yenye pointi moja Uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde.
    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Tunisia wote watakuwa ugenini kwa Libya na Guinea katika mechi zao za mwisho kuwania tiketi ya Urusi, huku kila mmoja akimuombea dua mbaya mwenzake.

    DRC yenye pointi saba itamenyana na Libya yenye pointi tatu Uwanja wa Stade Mustapha Ben Jannet mjini Monastir, Tunisia  wakati Guinea watakuwa wenyeji wa Tunisia Uwanja wa Septemba 28 mjini Conakry.
    Vikosi vya jana vilikuwa; Mali: Diarra, Wague, Traore, Kone, Fofana, Doumbia, Samassekou, Diarra, Bissouma/Haidara dk80, Niane/Coulibaly dk63, Traore/Djenepo dk40.
    Ivory Coast: Gbohouo, Aurier, Kanon, Bailly, Konan, Die/Sanogo dk46, Gbamin, Kessie, Kodjia, Cornet, Assale/Kalou dk67.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVORY COAST MGUU NJE, MGUU NDANI KOMBE LA DUNIA MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top