• HABARI MPYA

  Saturday, October 14, 2017

  ATLETICO MADRID NA BARCA, REAL NA GETAFE LA LIGA LEO

  RAUNDI ya nane ya Ligi Kuu Hispania, ijulikanayo tu kama La Liga ambayo huonyeshwa moja kwa moja katika Televisheni ya Azam inatarajiwa kuendelea leo.
  Mabingwa watetezi, Real Madrid wanatarajiwa kuwa na shughuli nyepesi Uwanja wa Coliseum Alfonso Perez mbele ya Getafe kuanzia Saa 11:15 jioni, wakati Athletic Club ya Bilbao itawakaribisha Sevilla Uwanja wa San Mames Barria kuanzia Saa 8:00 mchana na Deportivo Alaves wataikaribisha Real Sociedad Uwanja wa Mendizorroza kuanzia Saa 1:00 usiku.
  Shughuli pevu zaidi inatarajiwa kuwa Uwanja wa Wanda Metropolitano uliokarabatiwa, Atletico Madrid wakiikaribisha Barcelona kuanzia Saa 3:45 usiku.
  Baada ya kuisaidia Argentina kufuzu Kombe la Dunia, Lionel Messi anarejea kuipigania Barca kwenye La Liga  

  Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Lionel Messi akitoka kuisaidia Argentina kufuzu Kombe la Dunia mwakani, atakutana na Antoinne Griezmann ambaye naye ametoka kuisaidia Ufaransa kufuzu fainali za Urusi mwakani. 
  Raundi hiyo ya nane itaendelea kesho kwa Eibar kuikaribisha Deportivo La Coruna Uwanja wa Manispaa ya Ipurua, Girona na Villarreal Uwanja wa Manispaa ya Montilivi, Malaga na Leganes Uwanja wa La Rosaleda na Real Betis na Valencia Uwanja wa Benito Villamarin.
  Raundi ya nane itahitimishwa Jumatatu kwa mchezo kati ya timu ya Las Palmas na Celta de Vigo Uwanja wa Gran Canaria.
  Barcelona ndiyo wanaoongoza hadi sasa kwenye msimamo wa La Liga, wakiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi saba, wakifuatiwa na Sevilla pointi 16, Valencia na Atlético Madrid pointi 15 kila moja, wakati Real Madrid wapo nafasi ya tano kwa pointi zao 14 baada ya kucheza mechi saba pia. 
  Katika mchezo wa jana uliofanyika Uwanja wa RCDE mjini Cornella de Llobregat, wenyeji Espanyol walilazimishwa sare ya 0-0 na Levante.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ATLETICO MADRID NA BARCA, REAL NA GETAFE LA LIGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top