• HABARI MPYA

    Sunday, August 06, 2017

    MANYIKA NI MCHEZAJI MPYA HALALI WA SINGIDA, AACHANA NA SIMBA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MLINDA mlango mwenye kipaji, Peter Manyika amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Singida United baada ya kuachana na klabu yake, Simba.
    Awali Simba ilimruhusu Manyika kutafuta timu atakayokwenda kupata nafasi ya kudaka ili acheze kwa mkopo, lakini sasa klabu hiyo imekubali kumuachia moja kwa moja mchezaji huyo aondoke kama mchezaji huru.
    Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba, Manyika amesaini baada ya kumalizana kabisa na Simba na kuachana nayo.
    “Anakuja baada ya kusaini mkataba na sisi kufuatia kuachana kabisa na klabu yake, Simba. Hata tena mkataba na Simba,”amesema Sanga Festo.
    Peter Manyika anaondoka Simba kwenda kucheza kwa mkopo timu ambayo atakuwa chaguo la kwanza anusuru kipaji chake


    REKODI YA PETER MANYIKA SIMBA 

    Jumla ya mechi alizodaka: 51

    Mechi alizodaka bila kufungwa: 30

    Jumla ya mabao aliyofungwa: 34


    Simba iliachana na Manyika na kipa wake mwingine mdogo, Dennis Richard iliyempandisha kutoka timu B, baada ya kuwasajili kwa mpigo makipa namba moja na namba mbili wa timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula kutoka Azam FC na Said Mohammed kutoka Simba SC.  
    Manyika aliyesajiliwa Simba SC Julai mwaka 2014, amedaka jumla ya mechi 51 za mashindano tofauti, nyingi za kirafiki akifanikiwa kusimama langoni mara 30 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa huku akiwa amefungwa jumla ya mabao 34.  
    Singida United anakwenda kukutana na makipa wengine watatu, wakiongozwa na mkongwe Ally Mustafa ‘Barthez’ pamoja na Said Lubawa na Benedicto Tinocco, ambao wote ni mahiri pia. 
    Peter Manyika wakati anasaini Simba SC Julai mwaka 2014. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Said Tuliy 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANYIKA NI MCHEZAJI MPYA HALALI WA SINGIDA, AACHANA NA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top