• HABARI MPYA

  Friday, June 02, 2017

  TWIGA STARS KUCHEZA NA DUBAI ARUSHA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars kitaingia kambini Juni 7, mwaka huu kwa ajili ya kujiaandaa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu za wanawake za Dubai na nyingine kutoka nchini Kenya.
  Akitangaza kikosi cha timu hiyo leo, kocha Mkuu wa Twiga Stars, Sebastian Nkoma amesema kwamba upande wa makipa ni Elina Julius, Najiat Abbas, Fatuma Omary na Faraja Kimlola.
  Kocha wa Twiga Stars, Sebastaian Nkoma akizungumza na Waandishi wa Habari leo   
  Mabeki ni Wema Richard, Christina Daudi, Maimuna Hamisi, Annastazia Anthony, Silvia Mwacha, Esther Mayala, Eva Jackson, Sophia Mwasikili, Christina Panklasi na Asfati Kasindo.
  Viungo ni Dorisia Daniel, Grace Mbeyela, Amina Ally, Asha Hamza, Happy Hezron, Kevilis Kikumbi, Anna Hebron, Tatu Iddi, Stumai Abdallah, Herrieth Shija, Hamisa Athumani na washambuliaji Rehema Abdul, Asha Rashid ‘Mwalala’, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’, Veronica Mapunda, Fatuma Mustafa na Oppah Clement.
  Kocha Seba amesema kikosi hicho kitakaa kambini kwenye hosteli za Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam kwa muda wa siku 12, kabla ya kuelekea mjini Arusha kwa ajili ya michezo hiyo ya kirafiki.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS KUCHEZA NA DUBAI ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top