• HABARI MPYA

    Saturday, June 03, 2017

    RONALDO ANATAFUTA TAJI LA 20 LEO TANGU AANZE SOKA

    KABATI LA MATAJI LA CR7
    Ligi Kuu England (3): 2007, 2008, 2009
    Kombe la FA (1): 2004
    Kombe la Lig (2): 2006, 2009
    Ngao ya Jamii (1): 2007
    Ligi ya Mabingwa (3): 2008 - with United, 2014, 2016 - with Real Madrid
    La Liga (2): 2012, 2017
    Kombe la Mfalme (2): 2011, 2014
    Super Cup ya Hispania (1): 2012
    Super Cup ya UEFA (1): 2014 
    Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA (3): 2008 - with United, 2014, 2016 - na Real Madrid 

    Cristiano Ronaldo akiwa ana umri wa miaka 32 anarudi Cardiff leo kusaka taji la 20 miaka 13 baadaye tangu atwae taji la kwanza mjini humo akiwa na Manchester United 

    MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo leo ataingia kwenye Uwanja wa Millennium mjini Cardiff, Wales kusaka taji la 20 wakati timu yake, Real Madrid ikimenyana na Juventus katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Jiji la Cardiff si mahali haswa ambako Ronaldo alipoanzia soka, lakini ni sehemu ambayo alianzia kucheza mechi kubwa, fainali na kutwaa mataji.
    Dunia imebadilika mno kwa miaka 13 tangu Manchester United ilipoifunga Millwall, Ronaldo akifunga bao la kwanza kati ya matatu kwa kichwa. 
    Na leo akiwa ana umri wa miaka 32, Ronaldo anatafuta taji la 20 mbele ya Kibibi Kizee cha Turin, mechi ambayo akifanya vizuri tena haitakuwa ajabu akishinda tena tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Mwaka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO ANATAFUTA TAJI LA 20 LEO TANGU AANZE SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top