• HABARI MPYA

    Sunday, June 18, 2017

    NYAMLANI, MWAKALEBELA WAJITOKEZA KUJARIBU BAHATI URAIS TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Jumanne Nyamlani leo amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania Urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi wa Agosti 12, mwaka huu Dodoma.
    Nyamlani alikuwa Makamu wa Rais wa TFF, chini ya Rais Leodegar Chilla Tenga kati ya Desemba 14, mwaka 2008 na Oktoba 27, mwaka 2013.
    Akawa mpinzani mkuu wa rais wa sasa wa TFF, Jamal Emil Malinzi katika uchaguzi uliopita Oktoba 27, mwaka 2013, lakini akashindwa baada ya kupata kura kura 52 dhidi ya 72 za ‘mbabe wake’.
    Nyamlani anafanya idadi ya watu sita hadi sasa waliojitokeza kuchukua fomu za Urais, pamoja na Malinzi wengine ni Katibu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela, Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Madega, Makamu wa Rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia na Fredrick Masolwa.
    Athumani Nyamlani amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania Urais wa TFF katika uchaguzi wa Agosti 12, mwaka huu Dodoma

    Katika nafasi ya Umakamu wa Rais ni waliochukua fomu hadi sasa ni Mulamu Nghambi, Michael Wambura na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambao wanachama wa klabu ya Simba. Kaburu ni Makamu wa Rais wa Simba kwa sasa.
    Nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni waliochukua fomu leo hadi sasa saa 6.30 mchana ni Lameck Nyambaya, Omar Ali, Abdallah Mussa, Peter Steven, Said Tulliy, Ally Mussa, Mussa Kisoki, Salum Chama, Ephraim Majige, Elias Mwanjala, Saleh Alawi, Kaliro Samson, Vedastus Lufano, Kenneth Pesambili, Mbasha Matutu, Samuel Daniel, Dunstan Mkundi, Athumani Kambi, Shaffi Dauda, Golden Sanga, Charles Mwakambaya, Benista Rugola, Thabit Kandoro na Goodluck Moshi.
    Wengine ni James Mhagama, Hussein Mwamba, Sarah Chao, Issa Bukuku, Stewart Masima, Emmanuel Ashery, Abdul Sauko, Mussa Sima, Stanslaus Nyongo, Ayoub Nyenzi, John Kadutu, Baraka Mazengo, Khalid Mohamed, Mohamed Aden, Cyprian Kuyava na Saleh Abdul.
    Uchaguzi Mkuu wa TFF umepangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma wakati zoezi la kuchukua fomu litakamilika Juni 20, mwaka huu na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21 mkapa Juni 23.
    Juni 24 na 25, mwaka huu, kamati itafanya kazi ya kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo majina ya wagombea wakati Juni 26-28 zitakuwa siku za kupokea na kuweka mapingamizi kwa wagombea na Juni 29 mpaka Julai Mosi itakuwa kipindi cha kupitia mapingamizi yote na kufanya usaili.
    Kwa mujibu wa Kuuli, Julai 2-3 kitakuwa kipindi cha kuchapisha na kubandika matokeo ya usaili, Julai 4-7 na kipindi cha Sektretarieti kuwasilisha masuala ya Kimaadili kwenye Kamati ya maadili, Julai 7-11 ni kipindi cha kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya kimaadili.
    Julai 15-17 kitakuwa kipindi cha kukataa Rufaa kwa maamuzi ya  masuala ya kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF, Julai 18-22 itakuwa siku ya kusikiliza rufaa za maadili na Julai 23 mpaka Julai 25 itakuwa siku ya kutoa maamuzi ya Rufaa, Julai 26-28 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa dhidi ya kamati ya Uchaguzi kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, rufaa hizo zitasikilizwa Julai 29 mpaka Agosti 2.
    Wagombea watajulishwa matokeo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Agosti 5-6 itakuwa siku ya kuchapisha majina ya wagombea watakaoingia kwenye Uchaguzi huo na kampeni kwa wagombea zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata yaani Agosti 12 itakuwa siku ya uchaguzi wa viongozi wa TFF.
    Nafasi zinazogombewa ni Rais wa TFF, Makamu wa Rais pamoja na nafasi 13 za wajumbe TFF wanaowakilisha kanda 13 za Kagera na Geita; Mara na Mwanza; Shinyanga na Simiyu; Arusha na Manyara; Kigoma na Tabora; Katavi na Rukwa; Mbeya na Iringa; Njombe na Ruvuma; Lindi na Mtwara; Dodoma na Singida; Pwani na Morogoro; Kilimanjaro na Tanga na Kanda maalum ya Dar es Salaam.
    Fomu za Urais zinapatikana kwa Sh. 500,000, Makamu wa Rais Sh. 300,000 na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Sh. 200,000. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYAMLANI, MWAKALEBELA WAJITOKEZA KUJARIBU BAHATI URAIS TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top