• HABARI MPYA

  Friday, June 16, 2017

  MCHAKATO WA UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA LA WANAWAKE TANZANIA (TWFA)

  Na Mwandishi Wetu,  DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA), leo Juni 16, 2017 imetangaza rasmi Uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, George Mushumba amesema kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hizo zitaanza kutolewa Juni 19, mwaka huu na kwamba mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa 10.00 jioni. 
  Mushumba amesema kwamba nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji. Sifa ya elimu kwa wagombea wote ni kidato cha nne.
  Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi fomu zitanunuliwa kwa Sh 200,000 wakati nafasi za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji fomu zitapoatikana kwa Sh 100,000. Fomu zitapatikana ofisi za Hosteli ya TFF zilizoko Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa TWFA, Amina Kaluma (kulia) akihojiwa na mtangazaji wa TBC, Jesse John

  Ratiba kamili kuelekea uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:-
  Juni 23, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.

  Juni 24, 2017- Kamati ya Uchaguzi kutangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba au kanuni za TWFA.
  Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
  Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.
  Juni 29, 2017-  Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.
  Juni 30, 2017-  Usaili kwa wagombea waliotangazwa
  Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa
  Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa
  Julai 03, 2017-  Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa
  Julai 04, 2017   Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea
  Julai 04 hadi 07, 2017-Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili
  Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHAKATO WA UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA LA WANAWAKE TANZANIA (TWFA) Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top