• HABARI MPYA

    Monday, June 19, 2017

    MAYAY, KIGOGO TRA WAMVAA MALINZI URAIS TFF, MTEMI AJITOSA UMAKAMU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Mtemi Ramadhani na Ally Mayay Tembele leo wamechukua fomu za kuwania nafasi tofauti katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Agosti 12, mwaka huu Dodoma.
    Mayay kiungo na beki wa Yanga kati ya 1999 na 2005 amechukua fomu ya kuwania, wakati Mtemi aliyewika  Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shijja Richard naye kujitosa kuwania urais.
    Simba SC kati ya mwaka 1981 na 1985 amechukua fomu ya kuwania Umakamu wa Rais. Mayay atapambana na rais wa sasa wa TFF, Jamal Malinzi aliyekuwa Katibu wake wakati anacheza Yanga.
    Ofisa wa TRA, Shijja Richard akiwa ameshika fomu za kuwania urais wa TFF baada ya kuchukua leo

    Kwa ujumla mbio za kuwania uongozi wa TFF zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shijja Richard naye kujitosa kuwania urais.
    Shija ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado. 
    “Ni kweli nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi kuhusu mimi na kwa nini nimejitosa katika nafasi hii, tuvute subira wakati wa kampeni ukifika nitazungumza, ila kwa leo itoshe kuuthibitishia umma kwamba nimechukua fomu ya urais,” alisema Shija. 
    Mgombea huyo ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sheria za Kodi na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ana Stashahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Fedha kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam na Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Uhasibu Arusha (IAA). 
    Pia Shija amehudhuria mafunzo mbalimbali ya uandishi wa habari na ameandikia magazeti mbalimbali hapa nchini kuanzia mwaka 1997.
     Mgombea huyo aliwahi kuitumikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambaana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Kwa sasa ni Mhazini Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), akiwa pia amepata kuongoza klabu mbalimbali za mpira wa miguu kwa ngazi tofauti. 
    Mwaka 2008 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka wilayani Chato (CDFA), ambapo alisimamia usajili wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi ambao hata hivyo hakugombea. Pia Shija amepata kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Bukoba Veteran iliyopo mkoani Kagera. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYAY, KIGOGO TRA WAMVAA MALINZI URAIS TFF, MTEMI AJITOSA UMAKAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top