• HABARI MPYA

  Friday, June 02, 2017

  FDFD KUZIWEZESHA SERENGETI NA NGORONGORO HEROES

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MFUKO wa Maendeleo ya Soka (TFDF) unaandaa mpango kazi wa miaka kumi ijayo kuanzia 2017 hadi 2027, ambao utahakikisha zinapatikana rasilimali za kutosha.
  Hayo yamesemwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi alipokuwa anazungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam.
  Malinzi amesema mfuko huu ulianzishwa mahsusi na Mkutano Mkuu wa TFF mwaka 2015 kwa ajili ya kukusanya rasilimali za kuendeshea programu za mpira wa vijana na wanawake. 
  Amesema mfuko huu unajiendesha wenyewe chini ya Bodi yake inayoongozwa na Mwenyekiti, Tido Mhando.
  Amesema lengo la mfuko huo ni kuhakikisha timu za Taifa za vijana Serengeti Boys,Ngorongoro Heroes na Kilimanjaro Warriors zinaandaliwa vyema.
  “Timu yetu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars inaandaliwa na inafuzu kucheza fainali za Afrika za Wanawake mwaka 2018 huko Ghana  na hatimae kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2019 huko Ufaransa,” amesema.
  Malinzi ameongeza kwamba TFF inaamini  kutokana na jitihada hizo za kujenga vikosi imara vya vijana vya Serengeti Boys iliyoshiriki fainali za Afrika huko Gabon, Serengeti Boys itakayoshiriki Fainali za Vijana za Afrika nchini Tanzania mwaka 2019 na Kilimanjaro Warriors (U23)  itakayoshiriki hatua ya kufuzu kucheza Olimpiki Tokyo mwaka 2020.
  “Kwa pamoja kuanzia mwaka 2020 kikosi kipya cha  Taifa (Taifa stars) kitaanza kuonyesha uhalisia wa sura yake, kitalelewa na kitakomaa tayari kushiriki hatua za kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026, hatua hizi za kufuzu kucheza hizi fainali zitaanza mwaka 2024. Shime Watanzania tuunge mkono jitihada hizi, kwa pamoja inawezekana, fainali za Gabon zimetudhibitishia hivyo,”amesemaa Malinzi.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FDFD KUZIWEZESHA SERENGETI NA NGORONGORO HEROES Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top