• HABARI MPYA

  Thursday, May 11, 2017

  REAL MADRID YAKAMILISHA BIASHARA, YAIFUATA JUVE FAINALI LIGI YA MABINGWA

  Cristiano Ronaldo akishangilia na mfungaji wa bao lao, Isco dakika ya 42, Real Madrid ikifungwa 2-1 na wenyeji, Atletico Madrid usiku wa Jumatano Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabao ya Atletico yamefungwa na Saul Niguez dakika ya 12 na Antoine Griezmann kwa penalti dakika ya 16. Real inakwenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Bernabeu, mabao yote yakifungwa na Ronaldo na sasa itakutana na Juventus katika fainali Uwanja wa Principality mjini Cardiff, Juni 3, mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAKAMILISHA BIASHARA, YAIFUATA JUVE FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top