• HABARI MPYA

    Wednesday, May 24, 2017

    WAZIRI DK. MWAKYEMBE KUWALAKI SERENGETI BOYS LEO DAR

    Na Alfred Lucas, LIBREVILLE
    WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe leo Jumatano Mei 24, 2017 ataongoza viongozi na wanafamilia wengine wa michezo hususani mpira wa miguu kuilakini Serengeti Boys - timu ya soka ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa miaka 17.
    Serengeti Boys inatarajiwa kutua Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania leo saa 8:50 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini ikitokea Libreville, Gabon kupitia Johannesburg nchini Afrika Kusini.
    Mara baada ya kutua, timu itakwenda Hoteli ya Urban Rose kupata mapumziko angalau ya siku moja kabla ya TFF kuandaa utaratibu wa kuagana nao.
    Baada ya Mheshimiwa Waziri Dk. Mwakyembe kuthibitisha kutokea Uwanja wa Julius Nyerere kuilaki timu, Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema: “Tunamshuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kuwapokea vijana ambao sasa wanaunda kikosi kipya cha taifa cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 20.
    Waziri Dk. Harrison Mwakyembe leo ataongoza viongozi na wanafamilia wengine wa michezo hususani mpira wa miguu kuipokea Serengeti Boys

    “Kauli mbiu yao - ‘Ngorongoro Heroes kunyaga twende mpaka kufuzu fainali za AFCON u 20 mwaka 2019’, michezo ya kufuzu kwa hatua hiyo ya fainali za U-20 zitaanza Aprili, mwakani. Vijana hawa wataingia kambini tena mwezi Oktoba, mwaka huu na watacheza mechi ya kimataifa ya kujipima nguvu.
    “Mpira huwa haulali, unachezwa saa 24 katika wiki duniani ambako huanzia Januari hadi Desemba, likimalizika shindano hili linakuja jingine. Maumivu ya kufungwa huwa ni mafupi, mashabiki siku zote huwa wanafkiria mechi ijayo. Tujiandae na Qulifiers za 2019 AFCON u-20, haziko mbali.” amesema.
    Timu hiyo ya vijana ilikuwa jijini Libreville nchini Gabon kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ya vijana iliyofanyika katika miji miwili ya Libreville na Port Gentil ambako iliondolewa kwenye hatua ya makundi na Niger. 
    Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 na Niger katika mchezo uliofanyika Port Gentil, hivyo kufanya matokeo ya timu zote mbili yaani Niger na Tanzania kufanana kwa pointi, idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa tangu kuanza kwa fainali hizi za AFCON, Mei 15, mwaka huu.
    Serengeti Boys iliyokuwa Kundi B iliondolewa Kundi B iliondolewa na Niger iliyopenya kwenda hatua ya Nusu Fainali kwa faida ya kupata ushindi katika mchezo ambao umekutanisha timu hizo kwani Tanzania ilifungwa 1-0 katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi.  
    Kanuni hiyo ya mashindano ya CAF inajieleza kuwa matokeo ya ‘head to head’ kwa maana zinapokutana timu mbili zenye uwiano wa pointi na magoli matokeo huamualiwa kwa mshindi kupewa nafsi katika mchezo uliokutanisha timu hizo mbili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI DK. MWAKYEMBE KUWALAKI SERENGETI BOYS LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top