• HABARI MPYA

    Wednesday, May 31, 2017

    AUBAMEYANG SAFARI IMEIVA KUTOKA DORTMUND KWENDA PSG

    Pierre-Emerick Aubameyang anatarajiwa kuondoka Borussia Dortmund kuhamia PSG ya Ufaransa PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    TAKWIMU ZA AUBAMEYANG MSIMU WA 2016-17

    Mechi: 32
    Mabao: 31
    Pasi za mabao: 2
    Nafasi alizotengeneza: 26
    Takwimu hizi ni za Bundesliga pekee 
    MSHAMBULIAJI wa Pierre-Emerick Aubameyang ataondoka Borussia Dortmund na kujiunga na Paris Saint-Germain kwa dau la Pauni Milioni 61 kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa.
    Taarifa zimesema mshambuliaji huyo wa Gabon, ambaye amemaliza msimu kama mfungaji bora wa Bundesliga, amekubali mshahara wa Pauni 168,000 kwa wiki.
    Pia imeelezwa kwamba, Aubameyang atapata kiasi cha Pauni Milioni 5.25 kama ada ya kusaini mkataba wa kujiunga na vigogo hao wa Ligue 1. 
    Kwa mujibu wa taarifa hizo, ni mambo madogo tu ya kukamilishwa kabla ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 kuungana na Edinson Cavani na wenzake nchini Ufaransa.
    Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez imeelezwa naye ni mchezaji anayewaniwa pia PSG, lakini nyota huyo wa Chile anavutiwa zaidi na Manchester City na Bayern Munich.
    Aubameyang amewaambia Dortmund anataka kuondoka baada ya kumakuza msimu akiisaidia timu yake kuifunga Eintracht Frankfurt 2-1 katika fainali Jumamosi na kutwaa Kombe la Ujerumani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AUBAMEYANG SAFARI IMEIVA KUTOKA DORTMUND KWENDA PSG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top