• HABARI MPYA

    Friday, May 26, 2017

    MSUVA, KASEKE NA CHIRWA ‘WATUNDIKWA’ KWA KUMSHUGHULIKIA REFA

    Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI watatu wa Yanga, Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wamesimamishwa kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hadi kesi yao ya kumsukuma hadi kumuangusha refa Ludovic Charles itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Viungo hao washambuliaji walifanya kitendo hicho katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza, timu yao ikifungwa 1-0. 
    Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo kwamba uamuzi huo wa Kamati umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu. Kwa upande wake, refa Ludovic Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi dhidi yake ni kwa mujibu w Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
    Obrey Chirwa amesimamishwa na TFF baada ya kuhusika katika kumghasi refa kwenye mechi dhidi ya Mbao FC

    Yanga nayo kama klabu imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mechi hiyo, adhabu ambayo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu. 
    “Uamuzi huo umezingatia pia kuwa Yanga imekuwa ikirudia kosa hilo mara kwa mara,” amesema Lucas.
    Aidha, kutokana na timu zote mbili kutopita kwenye mlango rasmi wakati wa kuingia uwanjani katika, kila klabu imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48), wakati Yanga pia imepigwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kutoingia vyumbani kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo pia imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
    Yanga pia imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kupita mlango usio rasmi katika mechi hiyo iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
    “Yanga imepigwa faini ya sh. 1,500,000 (milioni moja na laki tano) kwa kutoingia vyumbani. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(8) ya Ligi Kuu. Vilevile klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikiana. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu,”amesema Lucas.
    TFF imesema mashabiki wa Yanga walivunja uzio wa ndani (fence) wa upande wa Magharibi wakati wakiingia uwanjani kusherehekea ubingwa wa timu hiyo. Hivyo, klabu ya Yanga imeagizwa kulipa gharama za uharibifu huo uliofanywa na washabiki wake, uamuzi ambao umezingatia Kanuni ya 42(3) ya Ligi Kuu.
    Nayo klabu ya Mbao FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani kushangilia baada ya timu yao kupata ushindi.
    Katika hatua nyingine, Lucas amesema Yanga na Mbeya City zote hazikupita kwenye mlango rasmi wakati wa kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyochezwa Mei 13, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo, kila klabu imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kitendo hicho, uamuzi ambao umezingatia Kanuni ya 14(48).
    Yanga imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kutoingia vyumbani kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo pia imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
    Mechi namba 225 kati ya JKT Ruvu na Majimaji iliyoshinda 1-0; Timu ya Majimaji haikuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo iliyofanyika Mei 13, 2017 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    Kutokana na timu hiyo kurudia kufanya kosa hilo, klabu ya Majimaji imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja). Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
    Mechi namba 230 (Kagera Sugar 2 Vs Mbao FC 0).
    Klabu ya Mbao imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 13, 2017 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA, KASEKE NA CHIRWA ‘WATUNDIKWA’ KWA KUMSHUGHULIKIA REFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top