• HABARI MPYA

    Wednesday, May 31, 2017

    SIMBA YATAKA KUMTEMA AGYEI IMSAJILI AISHI MANULA

    Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
    SIMBA inataka kumuacha kipa Mghana, Daniel Agyei ili imsajili kipa wa Azam FC, Aishi Manula.
    Na hiyo ni kufuatia habari za Aishi kutokubaliana na Azam kuongeza mkataba, baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa mwezi ujao.
    Uongozi wa Simba SC unaamini ukimpata Aishi hautakuwa na sababu ya kuingia gharama za ziada kwa kuendelea kuwa na kipa wa kigeni, Agyei aliyejiunga na Wekundu hao wa Msimbazi Desemba mwaka jana kutoka Medeama SC ya Ghana.
    Hata hivyo, wazo hilo linapingwa na baadhi ya viongozi wa Simba, wanaoamini Agyei ni bora zaidi ya Aishi na ndiye anayeIfaa klabu hIyo kwa sasa ikirejea kwenye michuano ya Afrika.

    Simba inafikiria kuachana na kipa Daniel Agyei ili imchukue Aishi Manula kutoka Azam FC

    Simba ilikata tena tiketi ya kurudi kwenye michuano ya Afrika, baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Jamhuri Dodoma Jumamosi iliyopita.
    Na kwa ushindi huo, Simba imekata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani na pia itafungua msimu ujao kwa kumenyana na mahasimu, Yanga SC katika mechi ya Ngao ya Jamii.  
    Simba ilicheza michuano ya Afrika kwa mara ya mwisho, mwaka 2013 na kutolewa na Recreativo de Lobolo ya Angola Raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa vipigo vya nyumbani na ugenini, ikifungwa 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na 4-0 ugenini.
    Na Agyei ameidakia Simba jumla ya mechi 25 za mashindano yote, akifungwa mabao 10 huku mechi 16 akidaka bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
    Alisajiliwa kuchukua nafasi ya kipa Muivory Coast, Vincent Angban ambaye naye pia aliachwa akiwa ana rekodi nzuri. 

    Daniel Agyei (kushoto) yuko hatarini kutemwa Simba kumpisha Aishi Manula

    REKODI YA DANIEL AGYEI SIMBA
    1. Simba 2-0 Polisi Moro (Hakufungwa kirafiki, Jamhuri)
    2. Simba 1-2 Mtibwa (Alifungwa mbili kirafiki Chamazi)
    3. Simba 2-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Mtwara)
    4. Simba 1-0 JKT Ruvu (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    5. Simba 1-0 Ruvu Shooting (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    6. Simba 2-1 Taifa Jang’ombe (Alifungwa moja Mapinduzi)
    7. Simba 1-0 KVZ (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi)
    8. Simba 0-0 Yanga (Hakufungwa dk90, Penalti 4-2 Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
    9. Simba 0-1 Azam FC (Alifungwa moja Fainali Kombe la Mapinduzi)
    10. Simba 0-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Jamhuri, Moro)
    11. Simba 2-0 Polisi Dar (Hakufungwa Kombe la TFF Uhuru)
    12. Simba 0-1 Azam FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    13. Simba 3-0 Maji Maji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Songea)
    14. Simba SC 3-0 Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    15. Simba SC 1-0 African Lyon (Hakufungwa Kombe la TFF Taifa)
    16. Simba SC 2-1 Yanga (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    17. Simba SC 2-2 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    18. Simba 1-0 Madini FC (Hakufungwa, Kombe la TFF Sheikh Amri Abeid, Arusha)
    19. Simba SC 1-2 Kagera Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Bukoba)
    20. Simba 0-0 Toto Africans (Hakufungwa Ligi Kuu Kirumba)
    21. Simba 1-0 Azam FC (Hakufungwa Nusu Fainali Kombe la TFF)
    22. Simba 2-1 African Lyon (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    23. Simba 2-1 Stand United (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    24. Simba 2-1 Mwadui FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    25. Simba 2-1 Mbao FC (Alifungwa moja Fainali Kombe la TFF, Dodoma)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YATAKA KUMTEMA AGYEI IMSAJILI AISHI MANULA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top