• HABARI MPYA

    Tuesday, May 30, 2017

    SHOSE KUZIKWA MOSHI IJUMAA, ATASAFIRISHWA ALHAMISI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MWILI wa marehemu Shose Fidels Alhamisi utasafirishwa kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yaatakayofanyika Ijumaa.
    Taarifa ya familia ya marehemu imesema kwamba mwili wa mpendwa wao, Shose utaagwa mapema Alhamisi kabla ya safari ya kuelekea Moshi tayari kwa maishi yake Ijumaa, ambayo yatafanyiak Uru.
    Shose alifariki dunia Jumapili mchana, muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, kufuatia ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 eneo la Dumila mkoani Morogoro.
    Shose Fidels atasafirishwa Alhamisi ukwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yaatakayofanyika Ijumaa

    Binti huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 na ushei, alikuwa pamoja na Nahodha wa Simba, Jonas Mkude kwenye gari hilo na watu wengine, wakitokea Dodoma, ambako jana timu yao ilitwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri.
    Ndani ya gari hilo walikuwepo pia wapenzi wengine wa Simba, Jasmin na Faudhia ambao wameumia na wamelazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro na hali zao zinaendelea kuimarika.
    Hii ndiyo gari iliyochukua uhai wa Shose (picha ndogo juu kulia)

    Mkude alirejeshwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi katika hospitali ya Muhimbili kabla ya mapema Jumatatu kuruhusiwa, wakati dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba anaisaidia Polisi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHOSE KUZIKWA MOSHI IJUMAA, ATASAFIRISHWA ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top