• HABARI MPYA

    Sunday, May 28, 2017

    NI MALI, AU GHANA KUBEBA NDOO YA U-17 AFRIKA LEO?

    Na Mwandishi Wetu, LIBREVILLE
    MALI itamenyana na Ghana leo Uwanja wa l’Amitie mjini Libreville, Gabon kujaribu kutetea ubingwa wao wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 barani Afrika.
    Unatarajiwa kuwa mchezo mkali na wa kusisimua, baada ya timu zote kuonyesha viwango vizuri kuanzia hatua ya makundi ya michuano ya mwaka huu.
    Na zote, Mali na Ghana zilifuzu hatua ya fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penalti kwenye mechi zao za Nusu Fainali.   
    Malin watatetea ubingwa wa U-17 Afrika mbele ya Ghana leo?
    Ni kipa Youssouf Koita ndiye aliyekuwa shujaa wa Mali Jumatano iliyopita baada ya kuwawezesha mabingwa hao watetezi kutinga fainali akiokoa penalti tatu na kuileta timu yake katika nafasi ya kurudia mafanikio yake ya Niamey miaka miwili iliyopita ilipoifunga Afrika Kusini 2-0 kwenye fainali.  
    Ghana nayo iliitoa Niger kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 0-0 kwenye Nusu Fainali nyingine Uwanja wa Port Gentil Jumatano. Niger na Guinea zitamenyana na kuwania nafasi yatatu leo pia.
    Ikumbukwe Ghana imetokea Kundi A ambako ilikuwa na Guinea, Cameroon na wenyeji Gabon, wakati Mali imetokea Kundi B ambako ilikuwa na Niger, Tanzania na Angola. Zote, Ghana, Mali, Guinea na Niger zimefuzu fainali za Kombe la Dunia la U-17 nchini India Oktoba mwaka huu.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI MALI, AU GHANA KUBEBA NDOO YA U-17 AFRIKA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top