• HABARI MPYA

    Friday, May 26, 2017

    REFA WA KESHO NI AHMED KIKUMBO

    Na Mwandishi Wetu, DODOMA
    REFA wa Dodoma, Ahmed Kikumbo ndiye atakayechezesha fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) kesho Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
    Fainali ya ASFC itazikutanisha Mbao FC na Simba kesho Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kuanzia Saa 10.00 jioni.
    Na Kikumbo atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon pia wa Dodoma wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Peter Temu wa Arusha. 
    TFF inazitakia timu zote, Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na Kamishna wao pamoja na wanafamilia wa mpira wa miguu, mchezo mzuri wenye fanaka kwa kila upande.
    Bingwa wa Kombe la TFF, atajinyakulia kitita cha Sh. Milioni 50 kutoka kwa wadhamini, Azam TV na pia ataiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REFA WA KESHO NI AHMED KIKUMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top