• HABARI MPYA

    Friday, May 26, 2017

    KAMUSOKO AREJESHWA TIMU YA TAIFA YA ZIMBABWE

    KIUNGO wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi yake kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 dhidi ya Liberia mwezi ujao.
    Kocha wa muda wa Zimbabwe, Norman Mapeza ametaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajiki ya mchezo huo wa Kundi G dhidi ya Liberia.
    Kikosi hicho ni makipa; Edmore Sibanda (CAPS United, Zimbabwe), Ariel Sibanda (Highlanders, Zimbabwe), Petros Mhari (FC Platinum)
    Thabani Kamusoko amerejeshwa timu ya taifa ya Zimbabwe kwa ajili ya mchezo dhidi ya Liberia mwezi ujao

    Mabeki: Denis Dauda (CAPS United, Zimbabwe), Partson Jaure, Qadr Amin (both Ngezi Platinum, Zimbabwe), Onesimo Bhasera (SuperSport United), Teenage Hadebe (Chicken Inn, Zimbabwe), Jameson Mukombwe (Black Rhinos, Zimbabwe), Erick Chipeta (Ajax Cape Town), Sydney Linyama (Black Rhinos)
    Viungo: Thabani Kamusoko (Yanga SC, Tanzania), Devon Chafa, Ronald Chitiyo (both CAPS United, Zimbabwe), Simon Shoko (FC Platinum, Zimbabwe), Kuda Mahachi, Danny Phiri (both Golden Arrows), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns), Marvelous Nakamba (Vittese Arnhem, Holland), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum, Zimbabwe), Ovidy Karuru (AmaZulu)
    Washambuliaji: Tendai Ndoro (Orlando Pirates), Evans Rusike (Maritzburg United), Knowledge Musona (KV Oostende) na Prince Dube (Highlanders, Zimbabwe).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMUSOKO AREJESHWA TIMU YA TAIFA YA ZIMBABWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top