• HABARI MPYA

    Wednesday, May 24, 2017

    SIMBA NA YANGA KUWANIA MILIONI 60 ZA SPORTPESA SUPER CUP

    RATIBA YA SPORTPESA SUPER CUP
    Juni 5, 2017
    Singida United Vs FC Leopard
    Yanga SC Vs Tusker FC
    Juni 6, 2017
    Jang`ombe Boys vs Gor Mahia
    Simba Vs Nakuru All Star
    NUSU FAINALI
    Juni 8, 2017
    Singida United/AFC Leopards Vs Yanga SC/Tusker FC
    Simba SC/Nakuru All Star Vs Jangombe Boys/Gor Mahia
    FAINALI
    Juni 11, 2017
    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya SportPesa imeandaa mashindano maalum ya soka yatakayojulikana kama SportPesa Super Cup yatakayoshirikisha timu za Tanzania, Zanzibar na Kenya.
    Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari kwamba, bingwa wa michuano hiyo atapata dola za Kimarekani 30,000 na nafasi ya kucheza dhidi ya timu ya England.
    Amezitaja timu hizo kuwa Simba SC, Yanga SC na Singida United kwa Tanzania Bara, Jang'ombe Boys ya Zanzibar, Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC za Kenya.
    Tarimba amesema kwamba michuano hiyo itaanza Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11 na itafanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
    “Tunatarajia mashindano haya yatakuwa changamoto nzuri kwa timu zote zitakazoshiriki na pia burudani nzuri kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini, hususan mashabiki wa timu zenyewe,”amesema Tarimba.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA KUWANIA MILIONI 60 ZA SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top