• HABARI MPYA

  Thursday, April 13, 2017

  TUNISIA YAMTUPIA VIRAGO KASPERCZAK

  KOCHA maarufu, Mpoland Henryk Kasperczak ameondolewa timu ya taifa ya Hispania tangu mwishoni mwa wiki.
  Tunisia, inayowania kucheza fainali za kwanza za Kombe la Dunia tangu mwaka 2006, imeachana na Kasperczak tangu Jumamosi
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 70, ambaye aliiongoza Tunisia kufika fainali ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 1996 kabla ya kuondoka nakarejea kazini mwaka 2015.
  Mpoland Henryk Kasperczak ameondolewa timu ya taifa ya Hispania tangu mwishoni mwa wiki

  Tunisia ilifungwa na kutolewa katika Robo Fainali kwenye Faubali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon na vipigo vya kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Cameroon na Morocco vilichangia kutupiwa virago kwa kocha huyo.
  Tunisia wanakabiliwa na mechi ya nyumbani na ugenini dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 kati ya Agosti na­ Septemba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TUNISIA YAMTUPIA VIRAGO KASPERCZAK Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top