• HABARI MPYA

    Thursday, April 13, 2017

    N'GOLO KANTE, HAZARD NA ZLATAN WAINGIA SITA BORA TUZO YA PFA

    N'Golo Kante aliingia Sita Bora kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo msimu uliopita akiwa anachezea Leicester City, lakini hakuingia Tatu Bora PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA PFA 

    Alexis Sanchez (Arsenal)
    Eden Hazard (Chelsea)
    N'Golo Kante (Chelsea)
    Romelu Lukaku (Everton)
    Zlatan Ibrahimovic (Man United)
    Harry Kane (Tottenham) 
    NYOTA wa Chelsea, N'Golo Kante na Eden Hazard wameingia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA).
    Kante, ambaye aliingia pia Sita Bora mwaka jana kuwania tuzo hiyo akiwa anachezea Leicester City, mabingwa wa Ligi Kuu England, hakufanikiwa kufika Tatu Bora, lakini mwaka huu anapewa nafasi kubwa ya kushinda.
    Wengine walioingia hatua hii ni Alexis Sanchez wa Arsenal, Zlatan Ibrahimovic wa manchester United, Romelu Lukaku wa Everton na Harry Kane wa Tottenham Hotspur.
    Wakati Kane wa Tottenham akiingia hatua huyo, mchezaji mwenzake Dele Alli hayumo licha ya chipukizi huyo wa kimataifa wa England kufanya vizuri msimu uliopita.
    Mchezaji mwingine ambaye anaweza kujiona ana bahati mbaya kwa kukosekana kwenye hatua hii ni mshambuliaji wa Sunderland, Jermain Defoe ambaye licha ya kuwa na umri wa miaka 34 sasa amewafungia mabao 14  Black Cats. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: N'GOLO KANTE, HAZARD NA ZLATAN WAINGIA SITA BORA TUZO YA PFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top