• HABARI MPYA

  Thursday, April 13, 2017

  KIPA WA MC ALGER AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA

  KIPA wa klabu ya MC Alger ya Algeria, Faouzi Chaouchi juzi alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia askari Polisi.
  Chaouch alidaka kwa dakika zote 90, Yanga ikiifunga 1-0 MC Alger Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania tiketi ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. 
  Chaouchi mwenye umri wa miaka 32, kipa wa zamani wa timu ya taifa amehukumiwa kwa kumpiga askari Polisi aliyekuwa anatafuta wachezaji kwenye mechi mjini Algiers Februari 7.
  Kituo cha Televisheni binafsi cha Echorouk kimeripoti kwamba mahakama katika wilaya ya Bir Mourad Rais mjini Algiers pia ilimtaka mchezaji huyo kulipa faini ya dinars 50,000, sawa na dola za Kimarekani 450.
  Mchezaji huyo alikuwa shujaa wa ushindi wa mechi ya mchujo dhidi ya Misri amnbao uliipeleka Algeria Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 Afrika Kusini.
  Faouzi Chaouchi juzi alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kumshambulia askari Polisi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA WA MC ALGER AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top