Tovuti Hii hutembelewa na zaidi ya watu 60,000 kila siku, kutangaza biashara yako na www.binzubeiry.co.tz,
Tuma maombi kwa barua pepe 4thebetter@gmail.com.
 • HABARI MPYA

  Monday, April 17, 2017

  SIMBA SC YAILIPUA RHINO 2-0 KIRAFIKI TABORA

  Na Steven Kinabo, TABORA
  SIMBA SC imewapa raha mashabiki wake wa Tabora, baada ya kuilaza timu ya Daraja la Kwanza, Rhino Rangers mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini humo. 
  Mabao yote ya Simba yalipatikana kipindi cha pili, la kwanza likifungwa na winga Shizza Ramadhani Kichuya kwa penalti na la pili likifungwa na mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.
  Simba iliwasili Tabora kwa mchezo huo wa kirafiki ikitoka Kanda ya Ziwa Victoria ambako ilikwenda kucheza mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikifungwa moja, sare moja na kushinda moja.
  Ilifungwa 2-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kabla ya kushinda 3-2 dhidi ya Mbao FC na kulazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Hata hivyo, Simba ilipewa pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa na Kagera kutokana na madai ya wapinzani wao kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
  Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Peter Manyika, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid/Hamad Juma, Novaty Lufunga, Jonas Mkude, Juma Luizio/Hijja Ugando, Said Ndemla/Frederick Blagnon, Pastory Athahans/Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na Mwinyi Kazimoto/Shiza Kichuya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Note: Only a member of this blog may post a comment.

  Item Reviewed: SIMBA SC YAILIPUA RHINO 2-0 KIRAFIKI TABORA Rating: 5 Reviewed By: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top