• HABARI MPYA

  Monday, April 17, 2017

  CHELSEA YATHIBITISHA JOHN TERRY ATAONDOKA MWISHONI MWA MSIMU

  John Terry ataondoka katika klabu yake kipenzi, Chelsea mwishoni mwa msimu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  MATAJI YA JOHN TERRY CHELSEA 

  LIGI KUU: 4 (2004-05, 2005-06, 2009-10, 2014-15)
  LIGI YA MABINGWA: 1 (2012)
  KOMBE LA FA: 5 (2000, 2007, 2009, 2010, 2012)
  EUROPA LEAGUE: 1 (2013)
  KOMBE La LIGI: 3 (2005, 2007, 2015)
  KLABU ya Chelsea ya England imethibitisha kwamba beki wake kati gwiji, John Terry ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka miaka 36 aliibukia kwenye akademi ya klabu hiyo kabla ya kuchezea kikosi cha kwanza kwa miaka 22 hadi sasa.
  "John Terry na klabu ya soka ya Chelsea leo kwa pamoja zinatangaza kwamba Nahodha wetu ataondoka kwenye klabu mwishoni mwa msimu," imesema taarifa ya klabu katika tovuti rasmi.
  "Kila mtu Uwanja wa Stamford Bridge angependa kuelezea hisia zake kwa John na kumtaki kila la heri katika maisha yake,".
  "John ametupa zaidi ya miongo miwili ya kujitolea kwa huduma za kipekee. Katika kipindi hicho amejisikia furaha kuvaa jezi ya Chelsea, jambo alilolifanya katika mechi 713 tanfu alipoanza mwaka 1998, akifunga mabao 66. 
  Ni mchezaji wa tatu kuichezea mechi nyingi klabu na amekuwa Nahodha wa Chelsea kwa rekodi kwenye mechi 578.
  Msimu huu hajatumika sana uwanjani, kwani zaidi amekuwa akiwahamasisha wachezaji wenzake wanaocheza kujituma kuiletea ushindi klabu hata inaelekea kutwaa ubingwa chini ya kocha Antonio Conte.
  Ameshinda Ligi ya Mabingwa, mataji manne ya Ligi Kuu ya England, Europa League, makombe matano ya FA na matatu ya Ligi. Tuzo zake 14 zinamfanya awe mtu aliyekusanya tuzo nyingi kwa muda wote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YATHIBITISHA JOHN TERRY ATAONDOKA MWISHONI MWA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top