• HABARI MPYA

  Sunday, April 09, 2017

  MKUTANO MKUU WA TFF AGOSTI 12

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKAO cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichofanyika Jumapili ya leo (Aprili 9, 2017) pamoja na mambo mengine, kimeamua Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo ufanyike Jumapili ya Agosti 12, 2017.
  Miongioni mwa ajenda katika mkutano huo, itakuwa ni uchaguzi mkuu wa TFF. Kwa mujibu wa Katiba, uchaguzi huo utachagua Rais wa TFF, Makamu Rais wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
  Katika hatua nyingine, TFF imeagiza klabu ya Lipuli ya Iringa ifanye uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wake.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) akiwa na Waziri wa Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati)

  Hatua hiyo ya TFF inafuatia kuufuatilia kwa muda mrefu mgogoro wa kiuongozi ndani ya klabu ya Lipuli FC ya Iringa.
  TFF imeitaka Kamati yake uchaguzi kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi huu na ufanyike kwa mujibu wa Katiba ya Lipuli FC iliyopitishwa Juni 22, mwaka 2014. Kamati ya uchaguzi ya TFF ndiyo itahakiki na kutoa orodha ya wapiga kura.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKUTANO MKUU WA TFF AGOSTI 12 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top