• HABARI MPYA

  Monday, April 10, 2017

  MANYIKA ANAANZA LEO SIMBA NA MBAO KIRUMBA

  Na Steven Kinabo, MWANZA
  KIPA Peter Manyika leo anaanza kwenye kikosi cha Simba kinachomenyana na wenyeji Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Manyika anaanza leo kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu msimu huu, baada ya kipa wa kwanza Mghana Daniel Agyei kufungwa bao la mbali wiki iliyopita na Mbaraka Yussuf, Simba ikifungwa 2-1 na wenyeji Kagera Sugar Uwanja Kaitaba, Bukoba.
  Pamoja na hayo, kocha Mcameroon Joseoh Marius Omog amemuanzisha Hamad Juma katika beki ya kulia, huku Mkongo Janvier Besala Bokungu akichezeshwa beki ya kati pamoja na Mganda Juuko Murshid.
  Peter Manyika leo anaanza dhidi ya wenyeji Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza

  Mghana James Kotei ameanzishwa katika nafasi ya kiungo mkabaji, wakati kiungo mchezeshaji leo ni Muzamil Yassin na washambuliaji ni Juma Luizio na Pastory Athanas, huku Shiza Kichuya akichezeshwa wingi ya kulia na kushoto Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
  Kikosi kamili cha Simba leo ni; Peter Manyika, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, 
  Juuko Murshid, Janvier Bokungu, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Juma Luizio, Mo Ibrahim na Pastory Athanas.
  Katika benchi wapo; kipa Daniel Agyei, viungo Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla na washambuliaji ni Ibrahim Hajib, Hajji Ugando, Frederick Blagnon na Laudit Mavugo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANYIKA ANAANZA LEO SIMBA NA MBAO KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top