• HABARI MPYA

  Wednesday, April 19, 2017

  KAZEMBE KOCHA MPYA TP MAZEMBE BAADA YA MFARANSA KUFUKUZWA

  NAHODHA wa zamani wa TP Mazembe, Pamphile Mihayo Kazembe amethibitishwa kuwa kocha mpya wa Les Corbeaux, akichukua nafasi ya Mfaransa, Thierry Froger.
  Kazembe mwenye umri wa miaka 40 sasa, amekuwa kocha wa muda wa mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa mwezi sasa, tangu akaimu nafasi ya Froger ambaye alifukuzwa Machi mwaka huu, kufuatia TP Mazembe kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Mihayo aliiwezesha TP Mazembe kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwishoni mwa wiki baada ya sare ya 0-0 dhidi ya mabingwa mara mbili Afrika, JS Kabylie ya Algeria na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-0. 

  Pamphile Mihayo Kazembe amethibitishwa kuwa kocha mpya wa TP Mazembe

  Mwenyekiti wa TP Mazembe na mfanyabiashara tajiri, Moise Katumbi amemtaka Mihayo kuhakikisha wanatetea taji lao la Kombe la Shirikisho.
  Mzaliwa huyo wa Lubumbashi, Mihayo anayafahamu vyema majukumu yake mapya na atapigania mafanikio ili kuendeleza rekodi yake nzuri ya tangu anacheza.
  Alikuwa Nahodha wa TP Mazembe wakati wanafika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA na kufungwa 3-0 na Inter Milan. 
  Mihayo anakuwa kocha wa kwanza asiye Mfaransa kufundisha TP Mazembe tangu mwaka 2012, kipindi ambacho Katumbi ameajiri na kufukuza Wafaransa watatu, wakiwemo Patrice Carteron, Hubert Velud na Froger. 
  Carteron alishinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2015 kabla ya mbadala wake, Velud kushinda Kombe la Shirikisho, lakini timu haikuwa katika kiwango kizuri hivyo Katumbi kumchukua Froger afanye mabadiliko, lakini kutolewa hatua za mwanzoni katika Ligi ya Mabingwa tena na timu ndogo, Caps United ya Zimbabwe kumlimfukuzish pia naye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAZEMBE KOCHA MPYA TP MAZEMBE BAADA YA MFARANSA KUFUKUZWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top