• HABARI MPYA

    Friday, April 14, 2017

    HASSAN KABUNDA: NATAKA KUFUATA NYAYO ZA BABA YANGA, LAKINI...

    KIUNGO Hassan Salum Kabunda ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa pili sasa akiwa na klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga.
    Katika dirisha dogo la usajili Desemba mwaka jana alitajwa kuwa kwenye mawindo ya klabu ya Simba, lakini dili hilo halikukamilika.
    Ungana na mwandishi wetu, Mahmoud Zubeiry katika makala ya mahojiano na mchezaji huyo, mtoto wa beki wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Kabunda ‘Ninja’ au Msudan. 
    Hassan Kabunda anataka kufuata nyayo za baba yake Yanga SC kama wataweza kumtimizia mahitaji yake

    Bin Zubeiry Sports – Online: Mkataba wako unamalizika lini Mwadui FC
    Hassan Salum Kabunda: Ligi ikiisha tu  
    Bin Zubeiry Sports – Online: Umekwishafanya mazungumzo ya mkataba mpya?  
    Hassan Salum Kabunda: Bado
    Bin Zubeiry Sports – Online: Kisheria upo huru kuzungumza na klabu nyingine. Je, umekwishafanya mazungumzo na timu nyingine yoyote labda? 
    Hassan Salum Kabunda: Bado kwa sababu sijataka kuongea mapema 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Lakini una taarifa zozote rasmi za timu yoyote kukutaka?
    Hassan Salum Kabunda: Nyingi tu 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Zitaje
    Hassan Salum Kabunda: Siwezi kuzitaja kwa sasa 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Kulikuwa kuna uvumi wa kwenda Simba usajili uliopita...ilikuwaje?
    Hassan Salum Kabunda: Sikutaka kukurupuka, niliamua na niliona mwenyewe na rehma za mama yangu nikaamua nikipige tena Mwadui      
    Bin Zubeiry Sports – Online: Mama yako anatakaje?   
    Hassan Salum Kabunda: Kwa sasa kaniambia nisaini kokote ninapotaka mimi
    Bin Zubeiry Sports – Online: Mwadui wako tayari kukuacha sasa uondoke?  
    Hassan Salum Kabunda: Hawapo tayari na hawatamani niondoke, ila tunakuja kwenye maamuzi ya mwisho, hayo ni yangu  
    Hassan Kabunda yuko tayari kufuata nyayo za baba yake Yanga iwapo klabu hiyo itamtimizia mahitaji yake 

    Bin Zubeiry Sports – Online: Ina maana hutaki kabisa kubaki Mwadui?

    Hassan Salum Kabunda: Hapana, kama wakinipa hela ninayoitka nitabaki  
    Bin Zubeiry Sports – Online: Baba yako alicheza Yanga        
    Hassan Salum Kabunda: Yah  
    Bin Zubeiry Sports – Online: Uliwahi kumuona akicheza Yanga?      
    Hassan Salum Kabunda: Hapana nilikuwa bado mdogo sana 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Umewahi kucheza timu ya watoto au ya vijana ya Yanga?    
    Hassan Salum Kabunda: Hapana
    Bin Zubeiry Sports – Online: Hujawahi kabisa kukanyaga Jangwani? 
    Hassan Salum Kabunda: Yah sijawahi
    Bin Zubeiry Sports – Online: Na hutamani kufuata nyayo za Ninja?    
    Hassan Salum Kabunda: Natamani, lakini ndiyo tunarudi pale pale kwenye makubaliano, kama tukielewana ninachotaka naenda 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Una Meneja?
    Hassan Salum Kabunda: Meneja wangu ni baba yangu wa kufikia, au Julio (Jamhuri Kihwelo)
    Bin Zubeiry Sports – Online: Simba sana huyo, atapenda uende Yanga?    
    Hassan Salum Kabunda: Tatizo makubaliano, mimi siangalii huyu Simba wala Yanga, naanglia maisha yangu nayatengeneza vipi, hivyo popote ninapokwenda kuongea nao mtu akikubali kiasi ninachotaka basi nasaini
    Bin Zubeiry Sports – Online: Na vipi ushindani wa namba Taifa Stars, itakuchukua muda gani kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza?   
    Hassan Salum Kabunda: Mpira nadhani unaujua, nahisi zamu yangu bado haijafka, lakini zamu yangu ikifika basi nitacheza tu. Mimi bado mdogo sana na naamini siku mwalimu atanipa nafasi nitapambana kadiri ya uwezo wangu kuhakiksha taifa letu tunaliweka katika kiwango kinachotakiwa
    Bin Zubeiry Sports – Online: Unapenda kuwa kama mchezaji gani?                        
    Hassan Salum Kabunda: Napenda kuwa kama Samatta, nifike alipofika yeye au zaidi ya hapo 
    Bin Zubeiry Sports – Online: Kama ni hivyo, huu ndiyo muda mwafaka kwako kwenda Ulaya kuanza kuyajenga pole pole. Unasemaje?                        
    Hassan Salum Kabunda: Ndiyo, na mimi nafikiria kwenda huko, ila mambo bado hayajatimia, nikifanikisha basi naweza kwenda
    Bin Zubeiry Sports – Online: Nipe historia yako kwa ufupi. Ulizaliwa lini, wapi umesoma shule zipi...                        
    Hassan Salum Kabunda: Nilizaliwa Juni 10, mwaka 1996 hapa hapa Dar es Salaam, Ilala. Nimesoma shule ya msingi Amana. Nilipomaliza shule ya msingi nikaanza mambo yangu ya soka na hapo nikachukuliwa na kituo cha kukuza kipaji cha DYOC cha kocha Ramadhani Aluko, ambao walinisomesha sekondari huku nikiwa kwenye hosteli zao. Nilikaa huko hadi nilipomaliza sekondari, tulikuwa tunacheza mashndano mengi mengi, wakati mwingine tulikuwa tunapelekwa IST (Shule ya Kimataifa ya Tanganyika) kucheza na Wazungu.
    Tulipomaliza huko tukaanza kucheza Ligi Daraj la Tatu. Kukawa na safari nyingi za nchi jirani  kama Kenya, Uganda kucheza mechi ambazo zilitujenga mno.
    Tuliporudi nikawa shuleni tu, nikaanza kucheza mashindano ya UMISETA (Umoja wa shule za Sekondari) na mimi nilikuwa Nahodha tukafanikiwa kutwaa Kombe. Nilipomaliza shule nilichukuliwa na timu ya mkoa wa Temeke na kwenda kucheza Copa Coca Cola nilipotokaa hapo nikaingia kwenye mashindano ya Airtel Rising Stard nikachaguliwa kwenda Afrika Kusini kwenye mashindano ya kimataifa.
    Niliporudi nikajiunga na African Lyon Under 20 nikacheza Uhai Cup, nilpomaliza nikaitwa Under 17 (Serengeti Boys) timu ya taifa nilipotoka huko nikarudi African Lyon nikacheza kama miaka miwil kisha nikaitwa tena timu ya taifa Under 20 nilipotoka hapo nikaenda Ashanti United, timu yangu ya nyumbani nikaanzia hapo kucheza Ligi Kuu. Nilicheza Ashanti hadi mwishoni mwa msimu iliposhuka nikajada Mwadui FC ambako nimecheza hadi kuonekana timu ya taifa.
    Salum Kabunda 'Ninja' (kushoto) waliosimama akiwa na kikois cha Yanga mwaka 1994 

    Bin Zubeiry Sports – Online: Mpo wangapi watoto wa Salum Kabunda

    Hassan Salum Kabunda: Tupo watano wote wa kiume na kila mtu ana mama yake. Ila wa kwanza mimi    
    Bin Zubeiry Sports – Online: Wengine? 
    Hassan Salum Kabunda: Wapo, mdogo wangu wa pili anaitwa Ally Kabunda nilikuwa naye Ashanti, aliwahi kuwa mfungaji bora kwenye Uhai Cup na kwa sasa yupo Cosmo wa tatu, Adam, wane Ibrahim wa tano Suleiman.
    Bin Zubeiry Sports – Online: Wengine? Klabu gani unaipenda Ulaya?      
    Hassan Salum Kabunda: Real Madrid na mchezaji anayenivutia ni Cristiano Ronaldo namkubali sana
    Bin Zubeiry Sports – Online: Nakuona unacheza kama kiungo mshambuliaji, je nafasi hiyo ni chaguo lako au ulichaguliwa?
    Hassan Salum Kabunda: Nafasi hii nilichaguliwa kocha Kime Poulsen baada ya kwenda Serengeti Boys, aliniambia mimi natakiwa kucheza winga na siyo mshambuliaji. Nikamsikiliza na ndiyo hadi leo nacheza nafasi hii
    Bin Zubeiry Sports – Online: Na unafurahia kucheza nafasi hiyo? 
    Hassan Salum Kabunda: Yah tena sana                        
    Bin Zubeiry Sports – Online: Mama yako wapi na anaitwa nani?                        
    Hassan Salum Kabunda: Rehema Mkali Said yupo Ilala, alikuwa anacheza Netiboli zamani   
    Bin Zubeiry Sports – Online: Hadi sasa soka imekunufaisha nini zaidi ya kusafiri nje ya nchi
    Hassan Salum Kabunda: Mambo mengi tu, maana ndiyo kazi yangu, ila kwa sasa siwezi kusema. Ila ninamshukuru Mungu. Alhamdulillah
    Bin Zubeiry Sports – Online: Ninashukuru Hassan, nadhani kwa leo inatosha
    Hassan Salum Kabunda: Asante anko. Nami ninashukuru.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HASSAN KABUNDA: NATAKA KUFUATA NYAYO ZA BABA YANGA, LAKINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top