• HABARI MPYA

  Saturday, April 15, 2017

  CAF YAPTISHA VIWANJA VYA UHURU, CCM KIRUMBA KUTUMIKA KIMATAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limevipitisha Viwanja vya Uhuru, Dar es Salaam na CCM Kirumba, jijini Mwanza kwa ajili ya michuano mbalimbali ya kimataifa ngazi ya klabu na timu za taifa.
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linachukua nafasi hii kuwapongeza wamiliki viwanja hivyo kwa namna walivyoweza kutunza hadi kukidhi matakwa ya CAF.
  Pongezi zinakwenda kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndio wamiliki wa Uwanja wa Uhuru na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza ambao ndio wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba.
  Viwanja hivyo vilikaguliwa hivi karibuni kwa nyakati tofauti na Mkaguzi wa CAF na FIFA, Maxwell Mtouga kwa kukagua vema na kutoa taarifa ambayo imefanya taasisi za CAF na FIFA - zinazoongoza mpira wa miguu, kupitisha viwanja hivyo kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya mechi za kimataifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAPTISHA VIWANJA VYA UHURU, CCM KIRUMBA KUTUMIKA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top