• HABARI MPYA

  Tuesday, September 20, 2016

  TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUANZA KUTUMIKA RASMI SIMBA NA YANGA OKTOBA 1 TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MFUMO wa kuingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa tiketi za Elektroniki utaanza rasmi kutumika Oktoba 1, mwaka huu katika mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga.
  Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye leo mchana katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Waandishi kadhaa wa habari michezo nchini leo wamepata fursa ya kupata maelezo ya kutumia huo mfumo mpya wa kieletroniki wa kuingia uwanjani baada ya kufungwa na kampuni ya Selcom iliyopewa zabuni hiyo.
  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo

  Nnauye alisema kabla ya mfumo huo wa kieletroniki kuanza kutumika rasmi katika mchezo wa watani, Simba na Yanga Oktoba 1 – utafanyiwa majaribio takribani mara mbili  au tatu.
  Aidha Waziri Nape pia amebainisha kuwa hakuna gharama za ziada ambayo Serikali imeingia katika ufungaji wa mfumo huo wa kieletroniki uwanjani hapo kwani hilo lilikuwa ndani ya mkataba wa wajenzi wa uwanja huo kampuni ya BCG.
  Kwa mujibu wa Meneja Mradi na mshauri wa mifumo wa Selcom Gallus Runyeta mfumo huo unaweza kupitisha watu  100,002 kwa saa tatu  hivyo kuondoa uwezekano wa kuwepo msongamano wakati wa kuingia uwanjani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUANZA KUTUMIKA RASMI SIMBA NA YANGA OKTOBA 1 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top