• HABARI MPYA

  Tuesday, September 20, 2016

  AZAM TV YALETA 'FULL DOWZII' KUTWA MARA TATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM Media imezindua promosheni yake mpya ya ' Full Dowzii Kutwa mara Tatu' ambapo mteja atapewa king'amuzi, dishi, remote na vifaa vyake vyote bure pamoja na kufungiwa kingamuzi hicho bure endapo mteja huyo atalipia 28, 000 kifurushi kikubwa cha Azam Play kwa mwaka mzima.
  Akizungumza na waandishi wa Habari jijini jana, katika ofisi za Azam media, Afisa Habari na Mawasiliano ya Nje, Irada Mahadhi amesema mteja ataweza kuokoa sh. 165,00 ikiwa ni gharama za vitu vyotevvya Azam Tv ilivyopatia bila kuvilipia na kupata channel zaidi ya 100 ndani ya kingamuzi hicho.
  Ofisa Habari na Mawasiliano ya Nje wa Azam TV, Irada Mahadhi (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari 

  Alisema kituo hicho kimeboresha kwa kiasi kikubwa sana idadi na viwango vya maudhiu yake ili kukidhi haja za wateja ambapi kila rika linaweza kupata kile kinachopendezewa kuanzia asubuhi, mchana hadi jioni na kuifanya burudani kuwa masaa 24 mfululizo kama dozi ya kutaa mara tatu.
  "Azam Tv ina vifurushi vitatu vya mwezi ambavyo ni Azam pure 15,000, Azam Plus 23,000 na kifurushi kikubwa cha Azam play 28,000, hiki ni kifurushi kikubwa ndicho kinahusika kwenye promosheni ambapo gharama zake kwa miezi 12 ni shilling 336,00 kwa maana ya 28,000 kila mwezi," alisema.
  Irada alisema promosheni hiyo ni mwezi mmoja ambapo mteja mpya badala ya kutoka sh. 135,000 kwa kununua kingamuzi hicho ikiwemo na ufundi atanunua kifurushi kwa sh. 28,000 ambapo atapewa kingamuzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM TV YALETA 'FULL DOWZII' KUTWA MARA TATU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top