• HABARI MPYA

  Friday, September 02, 2016

  SIMBA SC KUCHEZA NA POLISI DODOMA KESHO JAMHURI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC wanashuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kumenyana na wenyeji Polisi katika mchezo wa kirafiki.
  Simba imeweka kambi mjini Dodoma kufuatia mapumziko mafupi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kupisha mechi za mwisho za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
  Wachezaji wa timu kadhaa za Ligi Kuu, hususan Azam, Simba na Yanga wamekwenda na timu ya taifa, Taifa Stars nchini Nigeria kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi G dhidi ya wenyeji kesho. 
  Mohammed Hussein 'Tshabalala' ataiogoza Simba katika mchezo wa kirafiki kesho
  Wachezaji wengine kadha kutoka Azam, Simba na Yanga wa kigeni pia wameitwa kwenye timu zao za taifa hivyo kufanya ligi lazima isimame kwa muda.
  Na Simba SC imeona bora kuyatumia mapumziko hayo kwa kwa ziara ya michezo ya kirafiki Dodoma, kabla ya kushuka tena dimbani Septembna 7, kumenyana na Ruvu Shooting Uwanja w taifa, Salaam.
  Katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu, SImnba ilishinda 3-1 dbidi ya Ndanda FC kabla ya kulazimishwa sate ya 0-0 na JKT Ruvu juma lilillmiata.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUCHEZA NA POLISI DODOMA KESHO JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top