• HABARI MPYA

  Tuesday, September 20, 2016

  KILIMANJARO QUEENS MABINGWA CHALLENGE 2016, WAIPIGA KENYA 2-1

  Na Mwandishi Wetu, JINJA
  TANZANIA Bara imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Ufundi, Jinja.
  Shukraani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Stumai Abdallah dhidi ya moja la Kenya, lililofungwa na Christine Nafula.
  Kocha wa Kilimanjaro Queens, Sebastian Nkoma amefurahia ushindi huo na kuwapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri.
  Wachezaji wa Kilimanjaro Queens wakisherehekea baada ya kukabidhiwa Kombe lao

  Wachezaji wa Kilimanjaro Queens wakishangilia ushindi wao leo

  “Nimefurahi sana kwa matokeo haya, napenda nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu, tumedhihirisha ubora wetu hapa,”alisema Nkoma.
  Ikumbukwe, Kilimanjaro Queens iliingia fainali baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Uganda, wakati Kenya iliifunga 3-2 Ethiopia.
  Awali, Tanzania Bara iliongoza Kundi B baada ya kushinda kura ya sarafu kufuatia sare ya 0-0 na Ethiopia katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo, hivyo kufungana nayo kwa pointi na wasatani wa mabao kileleni. 
  Kilimanjaro Queens ilianza vizuri michuano hiyo kwa kuibamiza 3-2 Rwanda, mabao yake yakifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya wapinzani wao yalifungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.
  Kikosi cha Kilimanjaro Queens leo kilikuwa; Fatuma Omar, Donisia Daniel, Fatuma Bushiri, Amina Ally, Stumai Abdallha, Wema Richard, Maimuna Khamis, Anastazia Anthony, Fatuma Issa, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Asha Rashid ‘Mwalala’. 
  Benchi; Belina Julius, Fadhila Hamad, Fatuma Hassan, Sherida Boniphace, Fatuma Mustafa na Anna Hebron.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS MABINGWA CHALLENGE 2016, WAIPIGA KENYA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top