• HABARI MPYA

  Wednesday, May 04, 2016

  UCHAGUZI YANGA, FOMU KUANZA KUTOLEWA MEI 27

  Na Renatha Msungu, DAR ES SALAAM
  YANGA itaanza kutoa fomu kwa ajili ya wanachama wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia Mei 27 badala ya leo kama ilivyotangazwa awali na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit (pichani kushoto) amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, kwamba mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu hizo utakuwa ni Mei 29.
  Kiongozi huyo alisema kuwa baada ya zoezi hilo Kamati ya Uchaguzi itaanza kusikiliza pingamizi zitakazokuwa zimewasilishwa huku orodha ya mwisho ya wagombea waliopitishwa ikitarajiwa kutangazwa Juni Mosi.
  Aliongeza kuwa Juni Mosi hadi 4 itakuwa ni kipindi cha kampeni kwa wagombea waliopitishwa na uchaguzi mkuu utafanyika Juni 5 kwenye ukumbi utakaotangazwa hivi karibuni.
  Alisema kuwa uchaguzi huo utasimamiwa na TFF baada ya kushindwa kufanya uchaguzi tangu mwaka 2014 muda wa viongozi waliokuwa madarakani ulipomalizika.
  Kufanyika kwa uchaguzi huo kutatoa nafasi kwa viongozi wapya kusimamia usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na kufanya mabadiliko mengine ya katiba kwa kufuata maelekezo ya TFF.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UCHAGUZI YANGA, FOMU KUANZA KUTOLEWA MEI 27 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top