Kipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak akiokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich. Penalti hiyo ilitolewa baada ya Jose Gimenez kumchezea rafu Javi Martinez na Bayern Munich ikashinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Xabi Alonso dakika ya 31 na Robert Lewandowski dakika ya 74, huku la wageni likifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 53. Atletico inasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini licha ya sare ya jumla ya 2-2, baada ya wiki iliyopita kushinda 1-0 mjini Madrid na katika fainali itamenyana na mshindi wa jumla kati ya Real Madrid na Manchester City zinazorudiana usiku wa Jumatano Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza mjini Manchester PICHA ZAIDI GONGA HAPA
UNESCO yafunga mafuzo ya Mafundi Mitambo wa Radio za jamii 25
-
*Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu
UNESCO i...
16 minutes ago
0 comments:
Post a Comment