• HABARI MPYA

    Monday, May 09, 2016

    SHEREHE ZA UBINGWA YANGA KUFANYIKA MTWARA, KESHO WANACHEZA NA M.C.C.

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka leo asubuhi kwa ndege kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City (M.C.C.).
    Mchezo huo utafanyika kesho Uwanja wa Sokoine na Yanga pamoja na kuwa tayari imetwaa ubingwa, lakini  hawatakabidhiwa Kombe.
    Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba muda haukutosha kwa maandalizi ya Yanga kutawazwa kesho.
    Yanga wakisherehekea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita

    “Ni jana ndiyo Yanga imekuwa bingwa, sasa kutoka muda ule jioni haikutosha kwa wadhamini (Vodacom) kujiandaa kwa sherehe za ubingwa. Hivyo, hilo halitafanyika kesho,”amesema.
    Wambura amesema sasa Yanga watakabidhiwa Kombe lao katika mchezo dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda, Sijaona mjini Mtwara Mei 14, mwaka huu.
    Yanga imejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Simba SC kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Matokeo hayo yanamaanisha hakuna timu yoyote ya Ligi Kuu yenye uwezo wa kufikisha pointi 68 ambazo wanazo Yanga hadi sasa – na bila ubishi timu ya Jangwani imetetea ubingwa.
    Simba SC ina pointi 58 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kufikisha pointi 67 ikishinda mechi zake zote tatu zilizobaki, wakati Azam FC inaweza kumaliza na pointi 66. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHEREHE ZA UBINGWA YANGA KUFANYIKA MTWARA, KESHO WANACHEZA NA M.C.C. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top