• HABARI MPYA

  Saturday, May 21, 2016

  SERENGETI BOYS YAENDELEZA REKODI YA KUTOPOTEZA MECHI MICHUANO YA INDIA

  Na Mwandishi Wetu, GOA
  TIMU ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo imetoa sare ya mabao 2-2 na Malaysia katika mfululizo wa michuano maalumu ya kimataifa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka India (AIFF Youth Cup 2016 U-16) mjini hapa.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India mabao ya Serengeti yalifungwa Asad Ali Juma dakika ya 31 na Yohanna Oscar dakika ya 59 wakati ya Malaysia yamefungwa na Arif Suhaimi dakika ya 63 na Najmi Idhar dakika ya 68.
  Matokeo hayo yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi tatu, ikishinda moja na kutoa sare mbili na tayari imetinga Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAENDELEZA REKODI YA KUTOPOTEZA MECHI MICHUANO YA INDIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top