• HABARI MPYA

  Tuesday, April 19, 2016

  ZESCO KATIKA MTIHANI MWEPESI LEO NYUMBANI

  MECHI ZA MARUDIANO LIGI YA MABINGWA AFRIKA;
  Leo Aprili 19, 2016
  Zesco United Vs Stade Malien (Levy Mwanawasa, Saa 10:00 jioni)
  Ahly Tripoli Vs Asec Mimosas (Tunis, Saa 12:00 jioni)
  MO Bejaia Vs Zamalek (Unite Maghrebine, Saa 1:00 usiku)
  Kesho Aprili 20, 2016
  Al Ahly Vs Yanga SC (Borg el Arab, Saa 2:30 usiku) 
  ES Setif Vs El Merreikh (Mei 8, 45, Saa 2:00 usiku)
  TP Mazembe Vs Wydad Casablanca (TP Mazembe, Saa 10:30 jioni)
  ES Sahel Vs Enyimba (Olimpiki Sousse, Saa 2:00 usiku)
  Mamelodi Sundowns Vs AS Vita (Lucas Moripe, Saa 2:30 usiku)
  MATOKEO MECHI ZA AWALI
  Aprili 10, 2016  
  Enyimba 3-0 ES Sahel
  AS Vita 1-0 Mamelodi Sundowns
  Aprili 9, 2016  
  Wydad Casablanca 2-0 TP Mazembe
  Stade Malien 1-3 Zesco United
  Zamalek 2-0 MO Bejaia
  El Merreikh 2-2 ES Setif
  Asec Mimosas 2-0 Ahly Tripoli
  Yanga SC 1-1 Al Ahly
  Zesco United watakuwa na mtihani mwepesi leo nyumbani Ligi ya Mabingwa Afrika

  TIMU ya Zesco United ya Zambia inakutana na Stade Malien ya Mali katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Levy Mwanawasa, kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Zesco inatarajiwa kuwa na mechi nyepesi baada ya awali kuifunga Stade Malien 3-1 mjini Mali, maana yake leo hata kwa sare wanakwenda hatua ya makundi ya michuano hiyo.
  Mechi nyingine za leo ni kati ya Ahly Tripoli dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa mjini Tunis, Tunisia kuanzia Saa 12:00 jioni na 
  MO Bejaia dhidi ya Zamalek Uwanja wa Unite Maghrebine, kuanzia Saa 1:00 usiku.
  Mechi za kwanza baina ya timu hizo ASEC ilishinda 2-0 nyumbani na Zamalek ilishinda 2-0 nyumbani. Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya Al Ahly na Yanga SC Uwanja wa Borg el Arab mjini Alexandria kuanzia Saa 2:30 usiku, ES Setif na El Merreikh Uwanja wa Mei 8, 45, kuanzia Saa 2:00 usiku.
  TP Mazembe watakuwa wenyeji wa Wydad Casablanca Uwanja wa TP Mazembe, kuanzia Saa 10:30 jioni, Etoile du Sahel wataikaribisha Enyimba ya Nigeria Uwanja wa Olimpiki Sousse, kuanzia Saa 2:00 usiku na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini watakuwa wenyeji wa AS Vita Uwanja wa Lucas Moripe, kuanzia Saa 2:30 usiku.
  Mechi za awali Enyimba ilishinda 3-0 nyumbani, AS Vita ilishinda 1-0 nyumbani, Wydad Casablanca ilishinda 2-0 nyumbani, El Merreikh ililazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Yanga SC ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZESCO KATIKA MTIHANI MWEPESI LEO NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top