• HABARI MPYA

    Tuesday, April 19, 2016

    KILA LA HERI AZAM FC, MUNGU IBARIKI TANZANIA

    MECHI ZA MARUDIANO KOMBE LA SHIRIKISHO
    Leo Aprili 19, 2016
    Esperance Vs Azam (Novemba 7 Rades, Saa 2:00 usiku)
    Stade Gabesien Vs Zanaco (Olimpiki Gabes, Saa 9:30 Alasiri)
    Sagrada Esperanca Vs Vita Club Mokanda (Sagrada Esperanca, (Saa 10:30 jioni)
    Kesho Aprili 20, 2016
    Medeama Vs El Ahly Shandy (Sekondi-Takoradi  (Saa 10:30 jioni)
    SC Villa Vs FAR Rabat (Mandela, Saa 10:30 jioni)
    Misr Makkassa Vs CS Constantinois (Saa 1:00 usiku)
    Enppi Vs C.F. Mounana (Petro Sport, Saa 1:00 usiku)
    Kawkab Marrakech Vs Mouloudia D'oran (Grand Marrakech, Saa 3:00 usiku)
    Wachezaji wa Azam FC baada ya mazoezi yao ya jana Uwanja wa Novemba 7, mjini Tunis

    Na Mwandishi Wetu, TUNIS
    AZAM FC wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Rades na marefa kumenyana na wenyeji Esperance ya Tunisia katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
    Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Morocco ambao ni Redouane Jiyed atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Mouhib Abdallah Filali na Essam Benbaoa.
    Azam FC inahitaji kuulinda ushindi wake wa kwenhye mchezo wa kwanza wa 2-1 Dar es Salaam ili kusonga mbele katika mchujo wa kuwania kupangwa makundi ya ligi ndogo ya michuano hiyo.
    Kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart John Hall hana uhakika wa kumtumia winga wake machachari, Farid Mussa katika mchezo dhidi ya Esperance usiku wa Jumanne.
    Farid aliumia katika mazoezi ya Jumapili jioni mjini hapa baada ya kugongana na beki Said Mourad na kwa bahati mbaya, akagongana na beki huyo huyo katika mazoezi ya siku iliyofuata na kujitonesha maumivu.
    “Jana (Jumapili) amegongwa na Mourad, na leo (Jumatatu) tena amegongwa na yule yule Mourad, sasa sina uhakika wa kumtumia. Kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa Daktari. Nitajua kesho,”amesema Hall akimaanisha atajua siku ya mchezo wenyewe (leo).
    Azam FC Jumapili imefanya mazoezi yake ya kwanza Uwanja wa hoteli ya Carthage Thalasso na Jumatatu ikafanya kwenye Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Rades, Tunis ambao utatumika kwa mchezo huo.
    Katika mchezo huo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC inahitaji sare ili kusonga mbele baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
    Na Farid Mussa alifunga bao la kwanza kabla ya kumsetia Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyefunga la pili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Azam ikitoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 nyumbani.
    Tayari Azam FC itawakosa wachezaji wake wanne wa kikosi cha kwanza, mabeki Shomary Kapombe, ambaye ni mgonjwa, Serge Wawa majeruhi, kiungo Jean Baptiste Mugiraneza anayetumikia adhabu ya kadi na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche majeruhi pia.  
    Kapombe alikosa mchezo wa kwanza pia Dar es Salaam, wakati Wawa aliumia dakika za mwishoni kwenye mchezo wa kwanza na Esperance na Kipre aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa.
    Iwapo itashinda, Azam itaingia kwenye kapu la mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, ikimenyana na moja ya timu nane zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Kila la heri Azam FC.
    Wachezaji wa kigeni wa Azam FC kutoka kulia Didier kavumbangu (Burundi), Allan Wanga (Kenya) na Kipre Michael Balou (Ivory Coast)

    MATOKEO MECHI ZA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO
    Aprili 10, 2016  
    Azam 2-1 Esperance
    El Ahly Shandy 0-0 Medeama
    Vita Club Mokanda 1-2 Sagrada Esperanca
    C.F. Mounana 0-2 Enppi
    Aprili 9, 2016  
    CS Constantinois 1-0 Misr Makkassa
    Mouloudia D'oran 0-0 Kawkab Marrakech
    Zanaco 1-1 Stade Gabesien
    Aprili 8, 2016  
    FAR Rabat 7-0 SC Villa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILA LA HERI AZAM FC, MUNGU IBARIKI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top