• HABARI MPYA

    Wednesday, April 20, 2016

    ZAMALEK, ZESCO, SETIF ZATINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

    KOCHA wa zamani wa Ligi Kuu ya England, Alex McLeish ameiwezesha Zamalek ya Misri kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumanne.
    Hiyo inafuatia timu hiyo ya Cairo kulazimisha sare ya 1-1 na Mouloudia Bejaia ya Algeria katuika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora na kusonga mbele kwa ushindi wa 3-1 baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani.
    Faouzi Yaya alimtungua kwa shuti la mpira adhabu kipa Mahmoud Abdel Rehim dakika ya 57 kuwaptia Bejaia bao la kuongoza.
    Lakini mfungaji wa kwenye mchezo wa kwanza, Ahmed Hamoudi akaisawazishia Zamalek zikiwa zimebaki dakika mbili baada ya kuwatoa mabeki na kumtungua kipa Chamseddine Rahmani.
    Zamalek imefuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika

    Huo ulikuwa ni mchezo mmoja kati ya mitatu ya marudiano iliyocheza Jumanne-- mechi za kwanza za michuano ya Afrika kuchezwa katikati ya wiki katika miaka 52 ya mashindano hayo ya CAF (Shirikisho la Soka Afrika).
    Maybin Mwaba alitiokea benchi na kufunga zikiwa zimesali dakika tisa kuipa Zesco United ya Zambia ushindi wa 2-1 dhidi ya Stade Malien ya Mali mjini  Ndola.
    Wenyeji wangeweza kupata ushindi mnono kama wa kwenye mchezo wa 3-1 mjini Bamako wiki mbili zilizopita kama wangetumia vizuri nafasi. Mabao ya Zesco yamefungwa na Mkenya, Jesse Were ambaye angeweza kupiga hat-trick kama si kutolewa.
    Washindi wa zamani, ES Setif ya Algeria wametoa sare ya 0-0 na El Merreikh na kusonga mbele kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Sudan.
    Michuano hiyo itaendeela Jumatano kwa mechi kati ya; TP Mazembe (DRC) v Wydad Athletic (Morocco), Ahly Tripoli (Libya) v Asec Mimosas (Ivory Coast), Al Ahly (Misri) v Yanga SC (Tanzania), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) v AS Vita Club (DRC) na ES Sahel (Tunisia) v Enyimba (Nigeria).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMALEK, ZESCO, SETIF ZATINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top