• HABARI MPYA

  Sunday, April 03, 2016

  VIPORO DAY; YANGA NA KAGERA, AZAM NA TOTO MWANZA

  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo, huku macho ya wengi yakielekezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Taifa, Dar es Salaam ambako timu zinazowania ubingwa zitakuwa kucheza mechi zao za viporo.
  Azam FC watakuwa wageni wa Toto Africans Uwanja Kirumba, Mwanza wakati Yanga watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar Uwanja wa Taifa.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo ni kati ya Stand United na Mgambo JKT Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, JKT Ruvu na African Sports Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda na Prisons Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Azam FC wapo CCM Kirumba, Mwanza leo kumenyana na Toto

  Mechi za jana, Mbeya City iliifunga 4-0 Coastal Union Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Mtibwa Sugar iliifunga Mwadui FC 2-1 Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
  Ikumbukwe Simba SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 57, baada ya kucheza mechi 24, ikifuatiwa na Yanga na Azam FC ambazo kila moja ina pointi 50 za mechi 21, wakati Mtibwa Sugar ina pointi 42 za mechi 23 katika nafasi ya nne na Prisons iliyocheza mechi 24, ina pointi 39. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIPORO DAY; YANGA NA KAGERA, AZAM NA TOTO MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top