• HABARI MPYA

  Tuesday, April 19, 2016

  STEWART APANGA VIUNGO WATANO DHIDI YA ESPERANCE LEO, MSHAMBULIAJI MMOJA TU

  Na Princess Asia, TUNIS
  KOCHA Muingereza wa Azam FC, Stewart John Hall amepanga viungo watano na mshambuliaji mmoja tu kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance.
  Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Rades, Tunis kuanzia Saa 1:00 usiku na Saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
  Na Stewart amewapanga viungo Kipre Balou, Ramadhani Singano ‘Messi’, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy na Farid Mussa na mshambuliaji mmoja tu, Nahodha, John Raphael Bocco.
  Sure Boy ni kati ya viungo watano wanaoanza leo dhidi ya Esperance 
   

  Kwa ujumla kikosi cha Azam FC kipo; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Ramadhani Singano ‘Messi’, Frank Domayo, John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy, Farid Mussa,  
  Katika benchi wapo; Mwadini Ali, Said Mourad, Himid Mao, Khamis Mcha, Mudathir Yahya, Allan Wanga na Dididr Kavumbangu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STEWART APANGA VIUNGO WATANO DHIDI YA ESPERANCE LEO, MSHAMBULIAJI MMOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top