• HABARI MPYA

  Tuesday, April 19, 2016

  ESPERANCE NA AZAM FC LIVE AZAM TV KUANZIA 'TATU JUU YA ALAMA'

  TELEVISHENI ya Azam itaonyesha moja kwa moja mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji Esperance na Azam FC ya Tanzania Uwanja wa Olimpiki Novemba 7, mjini Rades, Tunisia.
  Meneja wa kitengo cha michezo cha Azam TV, Baruwan Muhuza ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba mchezo huo utakaoanza Saa 1:00 usiku na Saa 3:00 kwa saa za Afrika Mashariki, utarushwa moja kwa moja kupitia chaneli ya Azam TWO.
  Azam FC inahitaji sare kuingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam. 
  Baruwan Muhuza (kulia) akiwa Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Tunis jana, ambako leo itapigwa mechi kati ya Esperance na Azam FC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ESPERANCE NA AZAM FC LIVE AZAM TV KUANZIA 'TATU JUU YA ALAMA' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top